Ijumaa, 12 Desemba 2014

UVUNAJI WA MBAO, WATEKETEZA MISITU LUSHOTO



Z
aidi   ya wananchi 1000 wanaoishi kuzunguka msitu wa asili wa Bombo makole uliopo wilayani hapa wapo hatarini kukosa maji  kutokana na tishio la kukauka kwa vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji kwa wananchi hao kutoka katika msitu huo.

Tishio hilo la kukauka kwa vyanzo vya maji linatokana na kasi ya uvunaji  haramu wa mbao kutoka katika msitu huo unaofanywa na wafanyabiashara kwa kushirikiana na maofisa misitu wasio waaminifu wanaodaiwa kutoa vibali vya kuvuna magogo katika msitu huo kwa kisingizio cha shughuli za maendeleoe.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi  kwa zaidi ya wiki mbili wilayani hapa,umebaini kuwa,halmashauri ya wilaya ya Lushoto kupitia amati ya uvunaji imekuwa ikitumia mwanya huo kushirikiana na wafanyabiashara uhumu msitu huo.

Msitu huo ambao upo chini ya Halmashauri ya wilaya ya Lushoto umekuwa kichocheo kikubwa cha upatikanaji wa maji kutokana na kusheheni miti ya asili inayowezesha upatikanaji wa maji kwa mwaka mzima .

Akizungumza, mwenyekiti wa kijiji cha makole kilichopo kata ya Kilole,Athuman Tupa,alisema kuwa kama hatua madhubuti hazitachukuliwa uuokoa msitu huo,wananchi wa vijiji hivyo wataathirika kwa kiwango kikubwa na ukosefu wa maji.

Alisema kuwa,licha ya halmashauri ya wilaya ya Lushoto kuwachagisha fedha wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule,wananchi wa maeneo hayo hawanufaiki na raslimali za msitu huo kutokana na kuwanufaisha watu waliopo nje ya eneo lao.

Naye diwani wa kata ya Kilole,Salehe Manyenya,alisema kuwa pamoja na uvunaji huo wa magogo kuendelea,shule nane za msingi zilizopo kuzunguka msitu huo,zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati licha ya halmashauri ya wilaya kudai kuwa magog hayo yanavunwa kwa ajili ya matengenezo ya madawati.

Alizitaja shule hizo kuwa ni MziMkuu, Kwekanga, Makole, Ngwelo, Kwemanoo, Hemtoye, Chaumba ba Kwedeghe ambazo baadhi ya wanafunzi wamekauwa wakisoma huku wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba huo wa madawati.

Hata hivyo ofisa msitu wilaya ya Lushoto,Rashirid Hassan alikataa kuzugumzia shutuma hizo kwak ile alichodai yeye si msemaji wa halmashauri licha ya nyaraka kuonyeshe kuwa yeye ndiye mmoja wa maofisa wa idara ya misitu ambao wamekuwa wakitoa vibali vya ununaji wa magogo.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo mwandishi anazo,desemba 2 mwaka jana ofisa misiti huyo alitoa vibali  viwili kwa watu waliotajwa kwa majina ya  Kumbula Mbangula na Bebwa G.Ludovick kwa ajili ya uvunaji wa aina ya mikaratusi vibali ambavyo wananchi hao wanadai kuwa vinatumika kwa ajili ya kukata miti ya asili na si mikaratusi.

Hata hivyo vibali hivyo vinaonyesha waliopewa wanaruhusiwa kukata miti kwa ajili ya shughuli za maenndeleo na shughuli binafsi vibali ambavyo havifafanui shughuli binafsi ni zipi  na shughuli za maendeleo ni zipi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni