Jumapili, 4 Mei 2014

KINANA ATOA SOMO PEMBA

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.Katika hobuba yake,Ndg. Kinana amewataka Wananchi wa Kisiwani humo,kutohadaika na Wanasiasa wanapita kila mahali kwa lengo la kulipotosha Taifa,hasa juu ya swala la Muundo wa Serikali katika Mchakato wa Katiba Mpya.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiendelea kuwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwapa somo wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiendelea kuzungumza.
Makamu Mwenyekiti UWT,Bi. Asha Bakari Makame akizungumza kwa msisitizo mkubwa na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
Vijana wa CCM, Fatma Juma Ramadhan (kushoto) na Halima Juma Hajj wakighani mashairi mazuri ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (hayupo pichani).
Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar,Ndg. Shaka Hamdu Shaka akizungumza machache na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

DIAMOND ANG'ARA TUZO ZA MUZIKI, AZOA SABA


Msanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz Usiku ya Jana May 3, 2014 amedhihirisha kuwa yeye ni msanii mkali kwa kuchukua tuzo saba katika Tuzo za Kilimanjaro 2014 (KTMA).

Diamond amejinyakulia tuzo zifuatazo:-
Msanii Bora wa Kiume,
Video Bora ya Mwaka.
Mtumbuizaji bora wa Muziki wa Kiume.
Wimbo Bora wa Afro Pop.
Wimbo Bora wa Mwaka.
Mtunzi Bora wa mwaka Kizazi Kipya.
Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana.

Hakika Diamond ameonyesha ukali wake na kuonyesha kuwa yeye ni bora zaidi na anapendwa na watu.


Msanii Diamond Platnumz akipokea mojawapo ya tuzo zake 7 alizozipata katika Tuzo za Kilimanjaro 2014 (KTMA).

Mshindi wa tuzo  (7) za Kilimanjaro
Music Awards,
Diamond Platnumz akiwa
katika pozi na mpenzi wake
Wema Sepetu.


Aidha Huu ndio Mpangilio wote wa WASHINDI WOTE WA TUZO ZA KTM 2014,MEI 03:-.

Tuzo la Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili vya Tanzania limeshindwa na… Bora Mchawi - Dar Bongo Massive.

Msanii Bora Chipukizi Anayeibuka ni Young Killer.

Wimbo Bora wa Zouk kwa 2014 ni... Yahya - Lady Jaydee.

Wimbo Bora wa Afro Pop ni Number One - Diamond Platinumz.

Kwa mwaka 2014, Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall ni... Chibwa Ft. Juru – Nishai.

Wimbo Bora wa Reggae ni Niwe na Wewe – Dabo.

Wimbo Bora wa Taarab kwa mwaka huu ni... Wasi Wasi Wako-Mzee Yusuf.

Tuzo la Kikundi Bora cha Taarab limeshindwa na Jahazi Modern Taarab.

Mwimbaji Bora wa Kike - Taarab ni... Isha Ramadhani.

Mwimbaji Bora wa Kiume - Taarab ni... Mzee Yusuf.

Washindi wa Wimbo Bora wa Kiswahili Bendi kwa mwaka 2014 ni... Ushamba Mzigo - Mashujaa Band.

Mwimbaji Bora wa Kike - Bendi ni Luiza Mbutu.

Mwimbaji Bora wa Kiume - Bendi ni Jose Mara.

Rapa Bora wa Mwaka - Bendi ni Ferguson.

Tuzo la Bendi ya Mwaka limeshindwa na... Mashujaa Band.

Mwimbaji Bora wa Kike - Kizazi Kipya imeenda kwa... Lady Jaydee.

Mwimbaji Bora wa Kiume - Kizazi Kipya kwa mwaka huu ni... Diamond Platinumz.

Wimbo Bora wa R&B - Closer - Vanessa Mdee.

Kikundi cha Mwaka cha Kizazi Kipya ni... Weusi.

Wimbo Bora wa Hip-hop kwa mwaka 2014 imechukuliwa na... Nje ya Box - Nikki wa Pili Ft Joh Makini na Gnako.

Tuzo la Msanii Bora wa Hip-hop limeenda kwa... Fid Q.

Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikishana ni... Muziki Gani - Ney Mitego Ft. Diamond.

Wimbo Bora wa Afrika Mashariki - Jose Chameleone – Tubonge.

Mtunzi Bora wa Mwaka - Taarab... Mzee Yusuf.

Mtunzi Bora wa Mwaka - Bendi... Christian Bella.

Mtunzi Bora wa Mwaka - Kizazi Kipya imeenda kwa... Diamond.

Mtunzi Bora wa Mwaka - Hip-hop ni... Fid Q.

Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka - Bendi – Amoroso.

Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka - Kizazi Kipya ni... Man Water.

Hall of Fame - Individual - Rehan Bitchuka.

Hall of Fame - Institution - Masoud Masoud.

Video Bora ya Muziki ya Mwaka - Number One - Diamond Platinumz.

Wimbo wa Mwaka.... Number One – Diamond.

Mtumbuizaji Bora wa Kike wa Muziki... Isha Ramadhani.

Mtumbuizaji Bora wa Kiume wa Muziki... Diamond Platinumz.

WANAHABARI IRINGA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA


Katibu  wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin wa pili  kulia  akiongoza  wanahabari na wananchi wa kata ya Ilala kwenda kufanya usafi wa mazingira   leo  wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.

Wanahabari  mkoa wa Iringa  wakiadhimisha siku ya uhuru wa  vyombo vya habari kwa kufanya usafi.
Hapa  wakiendelea  kuzoa takataka

Wananchi  waliounga  mkono jitihada hizo

Mitaa mbali mbali ya Ilala usafi  ukifanywa na  wananchi kuunga mkono siku ya uhuru wa vyombo vya habari  jana
Na Diana Bisangao ,Iringa

WANAHABARI  mkoa  wa  Iringa  waungana na  wakazi wa kata  ya Ilala katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa waadhimisha  siku ya uhuru wa  vyombo  vya habari duniani kwa    kufanya usafiri wa mazingira  katika  kata  hiyo ya Ilala inayoongozwa na naibu  meya wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Grevas Ndaki.

Mbali ya  wanahabari  hao  kushiriki  kuzoa taka katika eneo hilo la Ilala  pia  wamefikisha neema kwa wananchi hao wa Ilala baada ya  kuwaombea chombo maalum cha  kuhifadhia taka (DAMPO) ambacho  walikuwa hawana na kulazimika kutupa katakata katika kiwanja cha mkazi mmoja wa eneo  hilo.

Wakizungumzia utaratibu  huo  wa wanahabari Iringa kujitolea  kufanya  usafi wa mazingira  baadhi ya  wananchi  wa kata  hiyo ya Ilala  walisema kuwa kilichofanywa na wanahabari  hao ni mfano wa kuigwa na  kuwa kwani  ni kwa  mara ya kwanza katika  kata  hiyo  wanashuhudia wanahabari hao  wakionyesha  mfano wa kushika vifaa vya usafi na kuzoa taka badala ya  kuandika pekee.

Alisema Amina Sanga  kuwa  baada ya  kusikia katika  vyombo  vya habari  jana  kuwa  wanahabari hao  wangefika  kufanya  usafi katika  eneo  lao  wengi  wao  walikuwa na  hamu ya  kushuhudia kama ni kweli  wanahabari  hao  watafika  kufanya usafi  ila  baada ya  kuwaona  wao kama  wananchi  walifarijika  zaidi .

Huku kwa  upande  wake  Husein Ally  alisema kuwa changamoto  kubwa  ya  usafi katika  eneo hilo ni kukosekana kwa chombo  cha kuhifadhia  taka na  hivyo kuwafanya  wananchi  kutupa takataka  eneo la uwanja  wa  mtu jambo ambalo kiafya ni hatari  zaidi kwani  wapo  baadhi ya  watoto  wamekuwa  wakishinda katika takataka hizo kuokota  uchafu  huo na kuchezea.

Hivyo  waliomba  wanahabari  hao  kuwasaidia  kuwaombea chombo  cha kuhifadhia  takataka  ili  kiweke eneo hilo na kila kinapojaa  basi gari la kubeba  uchafu la Manispaa kufika  na kuziondoa mapema.

Katibu  mtendaji  wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa wa Iringa (IPC)  Bw Francis  Godwin alisema  kuwa kitaifa  maadhimisho  hayo yamefanyika mkoani Arusha ambapo  mwenyekiti  wake Frank  Leonard amekwenda  kuwawakilisha  wanahabari  wa  mkoa  wa Iringa ambapo kauli mbinu kwa  mwaka  huu kitaifa ni  Uhuru wa Habari kwa maendeleo na  utawala  bora .

Godwin  alisema  kuwa  mbali ya kauli mbinu  hiyo ya kitaifa  mkoa  wa Iringa umeongeza kauli mbinu ya  pili  kwa ajili ya mkoa   huo mbali ya ile ya Taifa  pia wamejiongezea ile ya uhuru wa vyombo vya habari  na  usafi wa mazingira  ni jukumu letu sote .

Hivyo  alisema kuwa kutokana na heshima kubwa ya mkoa wa Iringa  iliyopata  kupitia Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa kwa kuwa ya  pili kiusafi  kitaifa  wao wameamua kuunga mkono jitihada hizo kwa kuhamasisha jamii  kufanya  usafi katika mji  huo .

Pia  kujitolea misaada mbali mbali kwa  kituo cha Yatima  cha DBL Mkimbizi  na kuwa  suala  hilo la usafi katika kata ya Ilala  limefanyika kama  sehemu ya  kuihamasisha  jamii  kuendelea  kufanya usafi katika maeneo yao .

Aidha  aliomba uongozi wa Manispaa kuunga mkono  jitihada hizo kwa  kuweka Dampo eneo hilo la Ilala ili kuwawezesha  wananchi hao kuwa na sehemu ya kuhifadhi takataka.

Afisa  msimamizi  wa  wahudumu wa usafi  katika Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Aron Mafumiko  mbali ya kuwapongeza wanahabari  hao kufika kufanya usafi  pia  alikubali kuweka dampo la kudumu eneo hilo la Ilala  kama  sehemu ya kuunga mkono jitihada za wanahabari hao mkoa wa Iringa.