Jumatano, 4 Februari 2015

RAIS GAUCK KATIKA SIKU YA PILI YA ZIARA, TANZANIA



Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, anaendelea na ziara yake nchini Tanzania, ambapo leo atatembelea visiwani Zanzibar, na kufanya mazungumzo na Rais Ali Mohamed Shein. 

Katika kukamilisha siku ya kwanza ya ziara hiyo jana usiku, Rais Gauck alikula chakula cha jioni alichoandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Ikulu ya Dar es Salaam. 

Gauck ameyasifu maendeleo ya kisiasa na kiuchumi ya Tanzania, ingawa amesema bado mengi yanapaswa kufanyika ili kuwawezesha wananchi wa kawaida. 

Amerejelea mtazamo wa Ujerumani kwa Tanzania kama taifa la Afrika Mashariki linaloinukia kwa kasi kiuchumi, hatua ambayo amesema inachangiwa na uwepo wa amani na utulivu wa kisiasa. 

Aidha, Rais Kikwete ameitaka Ujerumani kuimarisha uwekezaji wake kwenye sekta kadhaa zinazokuwa nchini Tanzania, hasa katika soko la utalii ambalo tayari Ujerumani imeonyesha muelekeo mzuri. 

Ziara hiyo itamfikisha Gauck hadi mkoani Arusha.

Jumanne, 3 Februari 2015

AWEKEWA MIKONO YA MTU MWINGINE, INDIA



Madaktari katika Chuo cha Tiba cha Amrita, Kochi huko India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa aina yake wa kupandikiza mikono mipya kwa binadamu aliyekatika viungo hivyo.

Upandikizaji huo uliofanyika Januari 12 na 13, ulifanikiwa kwa mara ya kwanza, baada mwanamume mwenye umri wa miaka 30, aliyekatika mikono katika ajali ya treni kuwekewa mingine. Mikono hiyo mipya ilichukuliwa kutoka kwa kijana wa miaka 24 aliyepata aliyefariki katika ajali ya gari.

Mkuu wa kitengo cha upasuaji katika chuo hicho, Profesa Subramania Iyer alisema: “Siku 14 baada ya upasuaji, mikono ilikubaliwa na mwili na ikaanza kujongea, yaani aliyepandikizwa aliweza kuisogeza huku na kule. Mgonjwa alitolewa chumba cha wagonjwa mahututi na huduma nyingine za kumchunguza ziliendelea.”

Daktari katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Hospitali ya Muhimbili (Moi), Profesa John Kahamba alisema hiyo si mara ya kwanza kwa upandikizaji wa mikono kufanyika duniani kwani na tofauti kubwa na upandikizaji wa figo au ini.

MIAKA 38 YA CHAMA CHA MAPINDUZI YAFANYIKA SONGEA



Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na kijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Maji Maji mjini Songea kwenye sherehe za  maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa  CCM.



Jumapili, 1 Februari 2015

DOLA LA KIISLAMU LAUA MWANDISHI WA HABARI



Wanamgambo wa itikadi kali wa dola ya kiislam-IS wadhihirika wamemuuwa  pia habusi wa pili wa Japan.Wamechapisha kanda ya video kupitia mtandao wa internet,inayoonyesha mwandishi habari Kenji Goto amekatwa kichwa.

Waziri wa ulinzi wa Japan Gen Nakatani amesema kanda hiyo ya video inaonyesha ni ya kweli.Katika kanda hiyo ya video anaonekana mtu aliyeficha uso wake akimuonya waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe "jinamizi limeshanza kuikaba Japan." 

Serikali mjini Tokyo ilitangaza kati kati ya mwezi uliopita wa january kutenga  dala milioni 200 kama msaada ambao si wa kijeshi kwaajili ya mapambano dhidi ya wanamgambo wa IS.Waziri mkuu Abe ameshasema hawatoupigia magoti ugaidi.

Rais Barack Obama wa Marekani amelaani kitendo hicho kuwa ni cha kinyama.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amelaani "mauwaji ya kishenzi" ya Goto na kuwataka wafuasi hao wa itikadi kali wawaachie huru haraka mahabusi wote wanaowashikilia.Jordan pia imelaani vikali kuuliwa mwandishi habari wa pili wa Japan Kenji Goto.
CHANZO: DW