Madaktari
katika Chuo cha Tiba cha Amrita, Kochi huko India wamefanikiwa kufanya upasuaji
wa aina yake wa kupandikiza mikono mipya kwa binadamu aliyekatika viungo hivyo.
Upandikizaji
huo uliofanyika Januari 12 na 13, ulifanikiwa kwa mara ya kwanza, baada
mwanamume mwenye umri wa miaka 30, aliyekatika mikono katika ajali ya treni
kuwekewa mingine. Mikono hiyo mipya ilichukuliwa kutoka kwa kijana wa miaka 24
aliyepata aliyefariki katika ajali ya gari.
Mkuu
wa kitengo cha upasuaji katika chuo hicho, Profesa Subramania Iyer alisema:
“Siku 14 baada ya upasuaji, mikono ilikubaliwa na mwili na ikaanza kujongea,
yaani aliyepandikizwa aliweza kuisogeza huku na kule. Mgonjwa alitolewa chumba
cha wagonjwa mahututi na huduma nyingine za kumchunguza ziliendelea.”
Daktari
katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Hospitali ya Muhimbili (Moi),
Profesa John Kahamba alisema hiyo si mara ya kwanza kwa upandikizaji wa mikono
kufanyika duniani kwani na tofauti kubwa na upandikizaji wa figo au ini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni