Wanamgambo wa itikadi kali wa
dola ya kiislam-IS wadhihirika wamemuuwa pia habusi wa pili wa
Japan.Wamechapisha kanda ya video kupitia mtandao wa internet,inayoonyesha
mwandishi habari Kenji Goto amekatwa kichwa.
Waziri wa ulinzi wa Japan Gen
Nakatani amesema kanda hiyo ya video inaonyesha ni ya kweli.Katika kanda hiyo
ya video anaonekana mtu aliyeficha uso wake akimuonya waziri mkuu wa Japan
Shinzo Abe "jinamizi limeshanza kuikaba Japan."
Serikali mjini Tokyo ilitangaza
kati kati ya mwezi uliopita wa january kutenga dala milioni 200 kama
msaada ambao si wa kijeshi kwaajili ya mapambano dhidi ya wanamgambo wa
IS.Waziri mkuu Abe ameshasema hawatoupigia magoti ugaidi.
Rais Barack Obama wa Marekani
amelaani kitendo hicho kuwa ni cha kinyama.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban
Ki-Moon amelaani "mauwaji ya kishenzi" ya Goto na kuwataka wafuasi
hao wa itikadi kali wawaachie huru haraka mahabusi wote wanaowashikilia.Jordan
pia imelaani vikali kuuliwa mwandishi habari wa pili wa Japan Kenji Goto.
CHANZO:
DW
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni