NI unyama,ndivyo unavyoweza kulielezea tukio la kupotea na hatimaye kupatikana akiwa amekufa mwanafunzi Humphrey Jackson Makundi(16)wa kidato cha pili katika shule ya sekondari binafsi ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro.
Mwanafunzi huyo alitoweka shuleni hapo Novemba 7 mwaka huu na mwili wake uliokotwa mita 300 kutoka ilipo shule hiyo ukiwa ndani ya korongo la mto Wona ukiwa na jeraha kichwani kuonyesha marehemu kabla ya kifo chake alipigwa na kitu chenye nchi kali.
Tayari watu 11 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano akiwamo mmoja wa wakurugenzi wa shule hiyo,Edward Shayo,walinzi,mama Lishe na wengineo huku polisi wakisisitiza wapo katika kiwango cha aslimia 50 katika uchunguzi wao.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishina msaidizi wa polisi(ACP),Hamisi Issah,amewaambia waandishi wa habari kuwa,hakuna atakayeachwa katika uchunguzi huo na ukikamilika na wahusika kubainika sheria itachukua mkondo wake.
Taarifa ya kutoweka kwa mwanafunzi huyo kwa mujibu wa kamanda Issah ilitolewa katika kituo cha polisi Himo Novemba 10 baada ya mwili huo kuchukuliwa na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospital ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,mawenzi.
Mwili huo ukazikwa chap chap katika makaburi ya Karanga yaliyopo moshi mjini huku wahudumu katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospital hiyo wakiwaeleza ndugu kuwa aliyepokelewa Hopsitalini hapo ni mtu mzima mwenye umri kati ya miaka 35 na 47.
“Hapa ukiangalia kuna utata,kwanza ni katika mazingira gani mwili huo ukazikwa chap chap bila hata kutoa muda wa watu kwenda kuangalia mwili ho kama ni wa ndugu yao ama la,kulikuwa na uharaka gani?”,amehoji mtoa taarifa wetu.
Taarifa kutoka kwa watu walioko karibu na shule hiyo zinapasha kuwa,kifo cha mwanafunzi huyo kinaacha maswali mengi kuliko majibu,huku baadhi ya wananchi wakihoji nani hasa aliyehusika na unyama huo dhidi ya mtoto huyo.
Humphrey ameondoka duniani na kushindwa kutimiza ndoto yake ya kuendelea na kidato cha tatu mwakani na hatimaye kidato cha nne mwaka 2019 na kifo chake kimetokea wakati huu wenzake wangali wakifanya mitihani ya taifa ya kumaliza kidato cha pili.
Ni tukio baya kuwahi kutokea katika siku za hivi karibuni mkoani Kilimanjaro na pia ni tukio linalotia simanzi kwa ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu na pia linawatia hofu wazazi wenye watoto wanaosoma shule za bweni na kutilia shaka usalama wa watoto wao.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,kamishna msaidizi wa polisi(ACP),Hamisi Issah,naye akapaza sauti kwa wamiliki wa shule binafsi na zile za serikali kwamba jukumu la kulinda usalama wa wanafunzi lipo mikononi mwao.
HUMPHREY ALIUAWA?
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na madaktari katika Hopsital ya Rufaa ya KCMC na kushuhudiwa na baba mzazi wa marehemu,Jackson Makundi,umebaini kuwa marehemu alipigwa na kitu chenye ncha kali na kupasua fuvu.
Baba mzazi wa marehemu,ameviambia vyombo vya habari kuwa,inavyoonekana katika uchunguzi huo,marehemu alikatwa na kitu cyenye ncha kali kiunoni,mgongoni,kwenye mapaja na mbavu mbili zilivunjika.
Anasema ni ukweli ulio wazi kuwa,mwanaye aliuawa na kwamba kifo chake kinatia shaka na kuvitaka vyombo vya uchunguzi kuwasaka wahusika wa mauaji ya mtoto wake mpendwa.
kuwata hivyo,utata zaidi juu ya tukio hilo umeibuka kutokana na madai ya wahudumu wa chumba cha kuhifahdi maiti katika Hopsital hiyo kuwaeleza ndugu wa marehemu kuwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni