CHAMA cha Wauguzi na
wakunga walio katika huduma binafsi Tanzania(PRINMAT)kimelalamikia urasimu
unaofanywa na serikali wa kuwanyima chanjo ya kuzuia maambukizi ya Virus vya
ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Malalamiko hayo yalitolewa hivi karibuni mjini moshi na mwenyekiti wa Chama
hicho,Keziah Kapesa katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye mkutano mkuu wa 17 wa
chama hicho unaoendelea mjini hapa.
Alisema zipo baadhi ya wilaya zimeshindwa kutoa friji za
chanjo pamoja na vitendanishi kwa vituo vya PRIMAT licha ya kwamba taarifa zote
za huduma hupelekwa ofisi za wagaga wakuu wa wilaya.
“Lakini kuna tatizo vituo kadhaa vya wauguzi kukosa fridge za
chanjo,wakati wakipata chanjo kutoka vituo vya jirani takwimu zinakwenda huko
halmashauri”,alisema.
Katika hotuba yake,mwenyekiti huyo amesema mbali na vituo
hivyo kukosa friji za chanjo,pia wauguzi hao na wakunga wamekuwa hawapati
mafunzo kazini kwa lengo la kuboresha huduma wanazotoa.
Amesema pamoja na kutopatiwa mafunzo,wakaguzi wamekuwa
wakifika kwenye vituo hivyo kwa ajli ya ukaguzi na kuhoji kwa nini vituo vya prinmat havitoi
huduma kwa njia iliyoboreshwa.
Chama hicho pia kimelalamikia hatua ya serikali kuvifungia
vituo vya pirnmat bila kutoa sababu za msingi
huku baadhi ya vituo vinavyofungwa vikiwa mbali na hospital za serikali
jambo ambalo kimedai linaweza kusababisha madhara makubwa kwa wagonjwa.
Kaimu mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya Afya,Dk.Dorothy
Gwajima alisema kuvifugia vituo vya afya
vilivyopo chini ya prinmat ni kuwanyima
huduma wananchi wasiokuwa na hatia.
Alisema prinmat ni wadua wakubwa wa wizara ya Afya kwani
wamesajiliwa na serikali na wanafuata miongozo yote ya serikali hivyo
kuvifungia vituo vyao ni jambo lisilokubalika.
Gwajima aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano huo,alisema kuna
matatizo yanayoweza kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya mazungumzo lakini baadhi ya
watumishi wa wizara ya afya wamekuwa wakikuza matatizo kwa makusudi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni