Jumatano, 4 Februari 2015

RAIS GAUCK KATIKA SIKU YA PILI YA ZIARA, TANZANIA



Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, anaendelea na ziara yake nchini Tanzania, ambapo leo atatembelea visiwani Zanzibar, na kufanya mazungumzo na Rais Ali Mohamed Shein. 

Katika kukamilisha siku ya kwanza ya ziara hiyo jana usiku, Rais Gauck alikula chakula cha jioni alichoandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Ikulu ya Dar es Salaam. 

Gauck ameyasifu maendeleo ya kisiasa na kiuchumi ya Tanzania, ingawa amesema bado mengi yanapaswa kufanyika ili kuwawezesha wananchi wa kawaida. 

Amerejelea mtazamo wa Ujerumani kwa Tanzania kama taifa la Afrika Mashariki linaloinukia kwa kasi kiuchumi, hatua ambayo amesema inachangiwa na uwepo wa amani na utulivu wa kisiasa. 

Aidha, Rais Kikwete ameitaka Ujerumani kuimarisha uwekezaji wake kwenye sekta kadhaa zinazokuwa nchini Tanzania, hasa katika soko la utalii ambalo tayari Ujerumani imeonyesha muelekeo mzuri. 

Ziara hiyo itamfikisha Gauck hadi mkoani Arusha.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni