Jumamosi, 31 Januari 2015

MWALIMU ABAKA MWANAFUNZI WAKE



Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ya Lyakrimu iliyopo wilaya ya Moshi Vijijini, Simon Lyimo akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wake wa kidato cha tatu katika shule hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo mapema leo  imesema Mwalimu huyo alimbaka mwanafunzi huyo jana saa 11.45 jioni baada ya mwalimu huyo kumwita mwanafunzi huyo kwenye moja ya chumba cha maabara shuleni hapo.

Aidha baada ya mwanafunzi huyo kuitikia wito wa mwalimu wake na kuingia katika chumba hicho, alijikuta akishikwa kwa nguvu na mwalimu huyo aliyeanza kumtomasa tomasa sehemu zake za mwili na kisha kumvuliwa nguo zake na hatimaye kuanza kubakwa.

Mwanafunzi huyo aliumizwa vibaya sehmu zake za siri, baada ya kufanya unyama huo alikimbia lakini nguvu ya sheria haikumwacha mwalimu huyo ambaye saa chache baadaye alitiwa mbaroni na anashikiliwa kwa mahojiano kabla ya kupandishwa mahakamani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni