Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingigira mjini moshi(MUWSA)
inaongoza kwa kiwango cha asilimia 98 katika usambaji wa huduma ya maji safi na
salama ikihudumia wananchi wapatao 187,108 katika kata zote 21 za Manispaa ya
Moshi.
Hayo yamo kwenye taarifa ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
iliyotolewa mwishoni mwa wiki kwa wajumbe wa kamati ndogo ya bunge Maji na
mifugo ambayo ilikuwaikitembelea na kuona utekelezaji wa miradi ya maji katika
mkoa huo.
Akitoa taarifa hiyo kwa kamati hiyo chni ya mwenyekiti wake,Seleman Moshi
kakoso,mhandisi wa maji mkoa,Injinia Immaculata Raphael,alisema kuwa hali ya
upatikanaji wa maji katika mji wa moshi ni nzuri kutokana na usdambaji mzuri
unaofanywa na MUWSA.
Alisema mkoa wa kilimanjaro wenye eneo la kilometa 13,209 za
mraba,eneo lenye maji ni kilometa za mraba 303 sawa na aslimia 2.3 na katika
muundo wa mabonde,mkoa uko katika bonde la mto Pangani na sehemu ndogo ya
wilaya ya Siha ikiwa bonde la kati.
kwa mujibu wa mhandisi huyo wa maji,mkoa wa
kilimanjaro unayo miradi ya maji 193 ambayo inapata maji yake kutokana na
vyanzo mbalimbali hususan chem chem,mito,maziwa,mabwawa,visima virefu na
vifupi huku mkoa ukifikia wastani wa aslimia 78 ya upatikanaji wa maji safi na
salama.
Alisema miradi mingi inatumia nguvu za mtiririko
katika kutoa huduma ya maji ambako milima ya Kilimanjaro na pare ndiyo vyanzo
vikuu vya maji hayo na kuongeza kuwa miradi ya visima virefu hutumia pampu
zinazoendeshwa kwa nishati ya umeme na mionzi ya jua wakati visima vifupi
utumia pampu za mikono.
kwa mujibu wa takwimu za mhandisi wa maji
mkoa,wilaya ya Hai inashika nafasi ya pili kwa kiwango cha aslimia 87 cha
usambazaji wa huduma ya maji safi na salama ikihudumia wananchi 188,868
ikifuatiwa na wilaya ya inayohudumia wananchi kwa kiwango cha aslimia 83.
Wilaya ya Moshi Vijijini yenye majimbo mawili ya
uchaguzi ya Vunjo na Moshi Vijijini,inashika nafasi ya nne katika usambaji wa
maji safi na salama kwa kiwango cha aslimia 75 ikihudumia wananchi 362,865 huku
ikifungamana na wilaya ya Rombo inayohudumia wananchi 202,886.
Mwanga inashika nafasi ya sita kwa wastani wa
aslimia 69 ikihudumia wananchi 94,015 huku wilaya ya same ikishika nafasi ya
sana na ya mwisho kwa wastani wa asilimia 68 ikihudumia wananchi 190,184,takwimu
hizo ni kutokana na idadi ya watu katika kila Halmashauri kwa mujibu wa sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012.
Mhandisi huyo wa maji mkoa alisema programu ya maji
na usafi wa mazingira vijijini inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri zote
baada ya kupokea fedha za utekelezaji tangu juni 2007 ambapo programu hiyo
itaendelea kwa awamu hadi mwaka 2025 ambapo awamu ya kwanza inatarajia
kukamilika mapema mweiz juni mwaka huu.
Alisema katika kutekeleza programu hiyo,mkoa
ulipokea kiasi cha sh,bilioni 14,282,025,772 kwa ajili ya miundombinu,usimamizi
na kujenga uwezo huku mkoa pia ukiidhinishiwa kiasi cha sh,Bilioni 6.4 katika
mwaka wa fedha 2014/15 kwa ajli ya kutekeleza na kusimamia miundombinu miradi
ya maji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni