
Makangula
ambaye ni mmiliki wa kampuni ya kutoa huduma za malipo ya kodi iitwayo Mshale
Investment & Tax Service, alihukumiwa Ijumaa katika Mahakama ya Wilaya na
Jaji Gray Miller kwa udanganyifu huo wa kuwasaidia wateja wake kughushi nyaraka
za kodi ya mapato, kwa mujibu wa tovuti ya click2houston.com.
Wakili
wa serikali nchini humo, Kenneth Magidson pamoja na Lucy Cruz, wakala maalumu
wa kitengo cha uchunguzi wa makosa ya kihalifu katika masuala ya mapato ya
Marekani, kwa nyakati tofauti waliiambia mahakama kuwa Makangula alimsaidia
mmoja wa wateja wake ambaye ni raia wa Marekani kutayarisha malipo ya kodi
yasiyo halali.
Sambamba
na kifungo cha mwaka mmoja na nusu, pia Makangula anatakiwa kulipa faini ya
Dola 51,645 sawa na Sh92.4 milioni.
Oktoba
15, mwaka jana, Makangula alikiri kosa hilo mbele ya hakimu Miller na kuwa
malipo ya kodi hiyo yalikuwa na udanganyifu katika vipengele kadhaa, yakiwamo
katika makadirio na idadi ya wategemezi wa mlipakodi, mambo yaliyosababisha
hasara ya Dola 9,731 za Marekani (Sh17.3 milioni).
Pia,
katika kesi hiyo, Makangula alikiri kuwa alimsaidia mteja wake kughushi kuwa
yeye ndiye mmiliki pekee wa biashara hiyo, hatua iliyosaidia watu wengine,
washirika wa mteja wake, wakwepe kulipa kodi.
Kampuni
ya Makangula inajishughulisha na huduma za ulipaji wa kodi, uhasibu, mfumo wa
ulipaji wa kodi za mapato, biashara za ardhi, kodi za majengo na ushauri wa
masuala ya kodi ya mapato.
CHANZO: MWANANCHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni