Alhamisi, 6 Novemba 2014

POLISI ALIYEMFUNGIA MWANAFUNZI GESTI ASHITAKIWA KIJESHI



J
eshi  la  Polisi nchini limemkamata na kumfungulia mashitaka ya kijeshi askari wake D.260 P/C.Godlisen anayetuhumiwa kumtumikisha katika vitendo vya ngono mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Okaoni iliyopo wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Mwanafunzi Agripina Andrew CHuwa akiwa amelala kitandani katika wodi namba tano katika Hospital ya Kibosho anakotibiwa majeraha yake baada ya kupata ajali ya pikipiki akiwa na  askari wa kituo cha Polisi Okaoni wakitokea moshi mjini kuelekea Kibosho,anayemuuguza ni mama yake mzazi Modesiana Chuwa.
Habari zilizopatikana hivi karibuni kutoka ndani ya jeshi la polisi mjini hapa zimedai kuwa,askari huo alifikishwa jana kwenye mahakama ya kijeshi ambako pia mwanafunzi huyo aliitwa kutoa ushahidi.

Septemba 21 mwaka huu  askari huyo anatuhumkiwa kumfungia kwenye nyumba ya kulala wageni  iitwayo KUWESE ya mjini hapa ambako anadaiwa kufanya naye mapenzi na baadaye kupata ajali mbaya ya pikipiki na mwanfunzi huyo kupata majeraha kadhaa sehemu mbali mbali za mwili.

Mwanafunzi huyo alikimbizwa katika Hospital ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu baada ya kupoteza fahamu lakini alihamishiwa katika Hospital ya Kibosho licha ya hali yake kuendelea kuwa mbaya kwa kile kilichoelezwa ni kukwepa macho ya watu wengi.

Hivi karibuni aliyekuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa  polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita  alikiri jeshi la polisi kufungua jarada la chunguzi juu ya tuhuma hizo na kwamba kama itabainika kuwa askari huyo alikwenda kinyume na maadili,hatua za kinidhamu zitachuliwa dhidi yake.

 Kamanda Koka alitetea hatua ya jeshi hilo kutochukua hatua mapema kuhjusiana na tukio hilo akidai kuwa,askari huyo alikuwa akiunguza jeraha alilolipata katika ajili hiyo na kwamba baada ya kupata nafuu aliagiza uchunguzi uanze haraka.

Pamoja na jeshi hilo kumfungulia mashitaka ya kijeshi askari huyo,taarifa kutoka kwa mmoja wa wazazi wa mwanafunzi hiyo zinadai kuwa,kuna juhudi za maksudi zinafanywa na askari wa jeshi hilo kutaka kukwamisha mashitaka hayo ya kijeshi  dhidi ya askari huyo.
Taarifa zinadai kuwa,polisi wa kituo kikuu cha polisi mjini moshi,wanajenga ushawishi kwa wazazi wa mwanafunzi huyo kutaka kulimaliza suala hilo kienyeji huku hali ya mwanafunzi huyo ikielezwa kuwa mbaya kutokana na miguu yake kuvimba.

Akizungumza juu ya mikakati hiyo ya kuharibu mwenendo wa mashitaka,baba mzazi wa mwanafunzi huyo,Andrew Chuwa,alisema  kuwa walishindishwa kutwa nzima nje ya kiuto cha polisi bila kuitwa kwenye mahakama ya kijeshi kutoa ushahidi,huku miguu ya mtoto wake ikiendelea kuvimba kutokana na kushida amesimama katika kituo kikuu cha polisi mjini hapa.

Alidai kuwa,polisi waliita ndungu wa askari anayetuhumiwa kumtumikisha mtoto wake katika vitendo vya ngono wakimshawishi suala hilo walimalize kienyeji  huku akiingiwa na hofu juu ya afya ya mtoto wake.

Mwanafunzi huyo alipelekwa katika Hospital ya mkoa ya Mawenzi kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kubaini kama aliingiliwa kimwili na askari huyo na hadi jana majibu ya uchunguzi huo yalikuwa hayajakabidhiwa kwa wazazi wa mwanafunzi huyo.

Naye Diwani wa kata ya Okaoni,ilipo shule hiyo,Morris Makoi,ametishia kuhamasisha na kuitisha maandamano makubwa ya wananchi hadi kituo cha polisi Okaoni kama Jeshi la Polisi litaendelea na danadana juu ya tukio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini hapa hivi karibuni,Makoi amesema tukio hilo limewafedhehesha wananchi wengi wa kata ya Okaoni na tarafa nzima ya Kibosho kutokana na kituo hicho kujengwa kwa nguvu za wananchi.

Akamtaka mkuu wa jeshi la polisi nchini(IGP)Ernest Mangu kufumua uongozi wote wa kituo hicho kuanzia mkuu wake wa kituo(OCS) na askari wote na kuleta askari waadilifu na wenye familia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni