Hali ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani
Mwanga si shwari kutokana na kuibuka kwa kundi linalotoa kadi za chama hichokwa
wanachama wapya bila utaratibu kwa misingi ya kujijenga kisiasa kuelekea
uchaguzi mkuu ujao na chaguzi za viongozi wa serikali za mitaa,vijiji na
vitongoji mapema mwezi ujao.
Habari zilizopatikana hivi karibuni kutoka wilayani mwanga na kudhibitishwa
na mbunge wa jimbo hilo,Profesa Jumanne Maghembe,zinadai kuwa tayari kadi
haramu 3,000 zimeingizwa wilayani humo na kugawanywa kwa wanachama wapaya bila
kufuata tararibu za kichama.
Akizungumza kutoka bungeni mjini Dodoma, Maghembe amedai
kuwa, wanaosambaza kadi hizo bado zinasambazwa kama njugu katika maeneo kadhaa
ya jimbo hilo na kukitaka chama hicho kuchukua hatua kwa wanaoendesha mchezo
huo mchafu .
Kadi zinatolewa kwa wingi katika maeneo ya
Kighare,Kilomeni,Kirongwe ambako taarifa zinadai kuwa zinatolewa bila utaratibu
ikiwamo wanachama kupewa bila kuomba na kutojadiliwa kwenye matawi .
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Juma Idd alisema kuwa tayari
wameagiza uchunguzi kufanyika na kubaini kama kadi hizo zinatolewa nje ya
utaratibu na kwamba watakaobainika kufanya hivyo watawajibishwa kwa mujibu wa
taratibu.
Hata hivyo mwenyekiti huyo alikwepa kuweka wazi juu ya mpasuko
uliopo ndani ya kamati ya siasa ya wilaya hiyo ambako taarifa zinadai kuwa
baadhi ya wajumbe wake hawasalimiani hali ambayo inaelezwa kuibua makundi
mawili .
Kundi moja ndani ya kamati hiyo ya siasa ni lile linalomuunga
mkono mbunge wa sasa Profesa Jumanne Maghembe na jingine likimuunga mkono
MNEC,Joseph Thadayo ambaye katika uchaguzi mkuu mwaka 2010,alibwagwa na
Maghembe kwenye kura za maoni.
Kutokana na mpasuko huo,baadhi ya wanaccm waliozungumza na
blog wamekitaka chama hicho makao makuu kuunda tume ya kuchunguza sakata
hilo kwa kile walichodai kuwa kamati ya siasa ya wilaya imeparanganyika.
Wamedai kuwa,kamati hiyo haiwezi kutoa matokeo mazuri ya uchunguzi
kutokana na mparanganyiko huo kwani hadi sasa wajumbe wa kamati hiyo
hawashirikiani hata katika shughuli za maendeleo hata kufikia hatua ya
kutozikana.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo,ndiye anayedaiwa kufadhili mpango
huo wa kusambaza kadi harahamu kwa lengo la kupanua wingo wa kisiasa na
kujiongezea wajumbe wengi wenye ushawishi mkubwa katika zoezi la upigaji wa
kura za maoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni