Suala la
ajira hapa nchini limeelezwa kuwa ndiyo tatizo kubwa katika jamii
huku wahanga wakubwa wakiwa ni vijana kutokana na kundi hilo
kuongoza kwa aslimia 61.7 ya watanzania wote.
MWANZILISHI/MTENDAJI MKUU WA TAASISI YA TANZANIA SME GROWTH CENTER,
VICTOR TESHA
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mwanzilishi na mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Tanzania SME Growth Center,Victor Tesha wakati akitoa elimu ya ujasiriamali kwa makundi ya kina mama na vijana katika kata za Uru Kishumundu na Uru Kaskazini.
Alisema kuwa kwa
mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kundi
la vijana ndilo linaloongoza kwa wingi kuliko makundi mengine ya
Wazee na Watoto ambako inaonyesha vijana kati ya umri wa miaka 15 – 35
wanafikia asilimia 61.7 .
Mtendaji huyo
mkuu wa Taasisi hiyo alikuwa alitoa elimu hiyo ikiwa ni mpango wa taasisi yake
kuwawezesha kina mama na vijana waliojiunga katika vikundi vya ujasiriamali
kunufaika na mikopo itakayotolewa na taasisi yake katika wilaya za Moshi
Vijijini na Mjini pamoja na mkoa wa Arusha.
Akitoa elimu
hiyo,Tesha alisema ufumbuzi wa tatizo la ajira litapungua na kufanikiwa
pale jamii itakapobaini kiini cha tatizo hilo na kiini hicho kimesambaa
kwa kiasi kipi suala ambalo linahitaji wadua binafsi na serikali kuangalia
namna ya kulitatua.
Katika kukabiliana na
tatizo hilo la ajira kwa vijana,mtendaji huyo alisema kuwa,vijana
wanatakiwa kuwa na mlengo wa mabadiliko kwa kuamini kuwa ajira si lazima
uajiliwe tu bali hata kwa kujiajiri kwa kufanya biashara ndogondogo na kuachana
na kasumba ya kuchagua kazi.
Alisema kwa
mujibu wa ripoti ya shirika la kazi dunia( ILO) ya mwaka 2011 inaonyesha kuwa
asilimia 78.8 ya vijana kote duniani hawakuwa na ajira, viwango vya
vijana waliokosa ajira ilifikia asilimia 12.6% mwaka 2013 na inategemewa
kupanda hadi kufikia 12.8% ifikapo mwaka 2018.
Aliongeza kuwa ripoti
hiyo imemzindua na kuwa na wazo la kutatua tatizo la ajira kwa kutafuta
taasisi ambazo zinaweza kutoa mikopo ya masharti nafuu kabisa ya
kuwawezesha vijana kujikwamua kimaisha kwa kujiajiri wenyewe.
Alisema watakaonufaika
na mikopo hiyo yenye riba nafuu ni vijana na kina mama waliojiunga katika
vikundi vya kuanzia watu kumi ambao watajiandikisha na vikundi vyao kutambulika
kisheria.
Chini ya mpango huo
kabla ya kunufaika na mikopo hiyo,vijana na kina mama watapewa mafunzo ya
kuwajengea uwezo kibiashara ili kupambana na matatizo yanayoweza kujitokeza,
kujua njia za kifasaha za kuendesha biashara .
Kwa mujibu wa
Tesha,mikopo hiyo itatolewa kwa mfumo wa vifaa badala ya pesa ambako kila
kikundi kitaainisha mahitaji yake kulingana na biashara watakayofanya kwa
pamoja ambako mikopo hiyo inatarajia kuanza kutolewa mwezi ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni