MAMLAKA ya maji
safi na Usafi wa Mazingira Moshi Mjini(MUWSA) inakamilisha utekelezaji wa
miradi mitatu ya maji ambayo itaondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji
safi kwa wananchi ifikapo desemba mwaka huu.
MKURUGENZI WA MUWSA, CYPRIAN LUHEMEJA
Hayo yamo kwenye taarifa
ya hali ya huduma ya maji safi iliyotolewa jana na mkurugenzi wa mamlaka
hiyo,Cyprian Luhemeja katika mkutano maalum na waandishi wa habari uliofanyika
kwenye ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo.
Miradi hiyo inahusisha
visima viwili vya CCP na Kili Tank pamoja na chanzo cha maji kilichopo mto
karanga ambacho maji yake yatazinufaisha kata za Pasua,Boma mbuzi,matindigana
na mabogini na maeneo ya katikati ya mji ambapo wananchi wapatao 20,000
watanufaika na mradi huo.
MABOMBA YA MAJI KATIKA HIFADHI SALAMA YA MUWSA
|
Alisema mradi huo wa
maji kutoka chemchem ya chanzo cha maji mto karanga unategemewa kuongeza mita
za ujazo 2,592 kwa siku katika mfumo wa kusambazia maji pindi mradi
utakapokamilika.
Kwa mujibu wa mkurugenzi
huyo,uzalishaji wa maji katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ni wastani wa
mita za ujazo, 34,944 kwa siku ikilinganishwa na mahitaji ya mita za ujazo
45,082 kwa siku.
Mamlaka hiyo pia
imefanya ukarabati wa kilometa 11.8 za mabomba katika mkakati wa kuhakikisha
maji yanayoongezwa kwenye mfumo wa kusambazia maji hayapotei kwa kupitia kwenye
maomba chakavu na hivyo kuwafikia wateja wengi zaidi.
AIR VALVE KATIKA CHANZO CHA MAJI, KARANGA MJINI MOSHI
|
Mkurugenzi huyo alisema
katika taarifa yake kuwa,matarajio ya mamlaka yake katika kipindi cha Oktoba
2014 na Juni 2015 ni kuanza ujenzi wa chemchem ya maji ya Ndesuo iliyopo
Kibosho wilaya ya Moshi vijijini katika mpango wake wa kuboresha zaidi huduma
ya maji safi.
Mpango mwingine wa
mamlaka hiyo ni kumalizia uchimbaji wa visima viwili vya maji vilivyopo kata ya
Longuo ambavyo mamlaka hiyo ilikabidhiwa na manispaa ya Moshi ikiwamo uwekaji
wa umeme,pampu,motor na mabomba.
Chini ya mpango
huo,mamlaka hiyo imelenga kufanyia ukarabati mtandao wa majisafi kwa
kilometa 14.9 pamoja na kufanyia upanuzi wa mtandao kwa kilometa 40.65 katika
sehemu mbalimbali za mji ambazo bado hazijafikiwa na mtandao.
WAANDISHI WA HABARI MJINI MOSHI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni