Uvamizi yanaofanywa na watu kwenye vyanzo vya maji
katika naeneo mbalimbali ya mji wa moshi yanatokana na matunda ya uongozi mbovu
wa watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia sheria za mazingira katika ofisi ya
mkurugenzi wa Manispaa ya moshi.
MEYA WA
MANISPAA YA MOSHI, JAPHARY MICHAEL
|
Tuhuma hizo zilitolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Moshi, Japhary Michael katika mkutano wake na waandishi wa habari uliolenga
kuelezea hali halisi ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa
manispaa hiyo na changamoto zinazoikabili mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira moshi mjini(MUSWA).
Meya huyo alisema kuwa upo ulegevu katika suala zima la
utekelezaji wa sheria ambao umesababisha watu kujenga karibu na vyanzo vya maji
kikiwamo chanzo cha maji cha Njoro ya |Dobi ambacho katika miaka 15
iliyopita,chanzo hicho kilikuwa moja ya vyanzo mhimu vya maji katika mji wa
Moshi.
Alisema kuwa chanzo hicho kimevamiwa na watu na kuweka makazi ya kudumu licha ya kelele za watetezi wa mazingira na kuongeza kuwa uvamizi huo umechangiwa na wenye mamlaka ya kusimamia sheria kutokuchukua hatua stahiki.
Kwa sasa chanzo hicho cha maji
hakitumiki kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuvamiwa na wananchi waliojenga
nyumba za makazi ambako wamekuwa wakitiririsha maji machafu yanayotokana na
kinyesi cha binadamu hali ambayo imekiweka chanzo hicho katika mazingira
hatarishi.
Kuhusu ujenzi holela unaoendela
katika baadhi a maeneo ya mji wa moshi,mtahiki meya huyo alisema kuwa,ujenzi
huo holela unashika kasi kutokana na usimamizi mbovu wa watendaji wa manispaa
ya moshi ambapo shutuma hizo alizielekezam oja kwa moja kwa idara ya mipango
miji ambayo ndiyo yenye wajibu wa kuhakikisha ujenzi holela unadhibitiwa.
Kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa moshi,meya huyo alisema kuwa,kwa sasa kuna jitihada kubwa zinazofanywa na MUWSA katika kutatua tatizo la maji kwa wakazi wam ji wa moshi huku maoneo yaliyokuwa yakikabiliwa namgao mkubwa wa maji kama vile Kiboriloni,Msaranga,pasua na Bomambuzi,maeneo hayo kwa sasa yanapata maji ya kutosha.
Kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa moshi,meya huyo alisema kuwa,kwa sasa kuna jitihada kubwa zinazofanywa na MUWSA katika kutatua tatizo la maji kwa wakazi wam ji wa moshi huku maoneo yaliyokuwa yakikabiliwa namgao mkubwa wa maji kama vile Kiboriloni,Msaranga,pasua na Bomambuzi,maeneo hayo kwa sasa yanapata maji ya kutosha.
Hata hivyo, Meya huyo alisema
kuwa,yapo baadhi ya maeneo ambayo bado hayapati maji ya uhakika na kwamba hiyo
ni changamoto kwa MUWSA kuhakikisha maeneo hayo yanapata maji ya kutosha huku
akielezea matumaini kwa wakazi wa kata za pasua na Bomambuzi ambao kwa sasa
wananufaika na mradi wa maji kutoka chanzo cha maji cha mto karanga.
Alitoa wito kwa wakazi wa manispaa
ya moshi kuwa mabalozi wazuri katika kusimamia ulinzi wa miundombinu ya maji
ikiwamo pia kuwa na matumizi mazuri ya maji safi na salama na kuzuia upotevu
huo wa maji.
Akizungumzia mfumo wa maji
taka,meya huyo alisema kuwa bado jamii ya wananchi wa mji wa moshi hawajapata
elimu ya kutosha juu ya kuunganishwa kwenye huduma hiyo na kuongeza kuwa hiyo
ni changamoto kwa MUWSA na manispaa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa
kuunganishwa katika huduma hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya MUWSA, mji
wa moshi umegaswanywa katika kanda kuu tisa ambako kila kanda inapata maji kwa
wastani wa saa 18 hadi 24 kutegemea na eneo lilivyo ambako katika kipindi cha
julai 2013 hadi sasa,wastani wa kutoa huduma ya maji kwa wateja umeimarika
kutoka saa 17.3 hadi saa 21.5.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni