MWANAISHA ATHUMANI PINDE
|
Usalama wa watanzania
wanaopelekwa nchini Dubai na Falme za Kiarabu kujaribu fursa za ajira upo
shakani kutokana na baadhi ya waajiri nchini humo kuwafanyia vitendo
visivyokuwa vya kibinadamu ikiwamo kupokwa pasi zao za kusafria na wengine
kujikuta wakiswekwa jela bila hatia.
Uchunguzi uliofanywana mtandao huu
kwa zadi ya mwezi mmoja sasa umebaini kuwa mbali na hilo,watanzania hao
wamejikuta wakifanya kazi kwa mali kauli pasipo kulipwa mishahara yao kama
ambavyo mikataba ya ajira inavyoosha.
Mmoja wa wahanga hao ni binti mwenye
umri wa miaka 36 ,Mwanaisha Athuman Pinde aliyezaliwa mkoani Morogoro
Novemba 25 mwaka 1978 kama pasi yake ya kusafiria inavyoonyesha.
Kwa mujibu wa nyaraka tulizonazo,Mwanaisha aliondoka Jijini Dar e s salaam kwenda Dubai Februari 17 mwaka huu na ndege ya shirika la ndege la Qatar yenye namba QR1350.
Uchunguzi umebaini kwamba alisafiri kwa msaada wa kampuni ya Bravo Job Centre Agency Ltd ya Jijijini Dar es salaam inayojihusisha na kuwatafutia fursa za ajira watanzania katika nchi mbalimbali na kupokelewa na wakala aitwaye Oriental Int,Labour Supply aliye na mkataba na Bravo.
Habari zinadai kuwa,baada ya binti huyo kupokelewa na kupelekwa kwa mwajili wake,alijikuta akiingia kwenye mgongano na mama mwenye nyumba na kulazimika kusitisha mkataba na kupelekwa kwa mwajili mwingine.

Kwa mujibu wa dada wa binti huyo,Zena
Athuman Pinde,mdogo wake huyo baada ya kupelekwa kwa mwajili mwingine aliipokwa
pasi yake ya kusafiria,simu pamoja na nyaraka nyingine huku akinyimwa kufanya
mawasiliano na ndugu zake.
Zena alisema
kuwa,mbali na hilo mdogo wake alikuwa akiishi bila kulipwa mshahara na pale
alipodai mshahara wake alijikuta akiambulia lugha chafu kutoka kwa mwajili
wake.
Kwa upande wake Mwanaisha akiongea na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutoka Abu Dhabi hivi karibuni,alisema alijikuta akiswekwa jela na maofisa wa polisi wa huku baada ya mwajili wake kumtelekeza na kushidwa kumrejesha nyumbani huku pasi pake akiwa ameishilikia pamoja na simu yake ya kiganjani.

Akizungumza kwa msaada wa ofisa wa
polisi mwenye asili ya Tanzania,mwanaisha amedai kuwa,chanzo cha kutofautiana
na mwajili wake ni hatua ya bosi huyo kutaka kumgeuza kitega uchumi kwa
kumbadilisha kazi za ndani na kutaka kumtumia katika biashara haramu.
Amedai baada ya
kugoma,alijikuta katika mgogoro na bosi wake na hapo upepo ukawa mbaya kwake
kwani alijikuta akipokwa kila kitu huku akiwa hajalipwa mshahara wake kwa muda
wa miezi sita sasa.
kwa mujibu wa
mwanaisha,tangu awasili Abu Dhabi,amekuwa hana mawasiliano na ndugu zake
kutokana na simu yake kuwa mikononi mwa bosi wake japo amefanikiwa kurejea
nyumbani kwa msaada wa ubalozi mdogo wa tanzania huko Abu Dhabi baada ya
kupatiwa hati ya muda ya kusafiria.
Akizungumza muda mfupi
baada ya kurejea nchini hivi karibuni na ndege ya shirika la ndege la kenya na
kupokelewa na ndugu zake,mwanaisha anadai kwa sasa anakamilisha tararibu za
kisheria kuifikisha mahakamani kampuni ya Bravo kwa kile alichodai kushindwa
kumsadia kupata haki zake.
Hata hivyo,msemaji wa
kampuni hiyo ya Bravo,Heri Mtemvu akizungumza na mtandao huu hivi karibini ofisini
kwake Keko Bora jijini Dar es salaam,alitetea hatua ya waajili huko Dubai ya
kuwapoka simu na pasi za kusafiiria watanzania wanaokwenda kufanya kazi huko.
Kwa mujibu wa
Mtemvu,hatua ya kupokonywa pasi na simu ni katika juhudi za kuzima majaribio ya
watumishi hao kutoroka pindi wanapopata vibali vya kuwawezesha kufanyakazi
nchini humo.
Mtemvu hata hivyo
alisema,kampuni yake ipo katika hatua za mwisho kwenda nchini Dubia kufuatilia
haki za mtanzania huyo ikiwamo mishahara yake pamoja na pasipoti yake ya
kusafiria ambayo ingali mikononi mwa tajili yake.
Kwa mujibu wa nyaraka
tuliozonazo,safari za watanzania kwenda katika nchi za falme za kiarabu
zimekuwa zikipata baraka kutokana wakala wa Huduma za ajira Tanzania(TaESA)
ambako mhusika hulipia ada ya sh,100,000 .
Nyaraka hizo zinaonyesha
kuwa,mwanaisha alikuwa na mkataba wa kufanyakazi za ndani kwa
mfanyabiashara Mohamed Saleh Yeslam Alameri ulioidhinishwa februari 5 mwaka huu
na kutiwa saini na Omary Mjenga kutoka TaESA.
"mtajwa hapo juu
mwenye pasipoti namba AB474488 amethibitishwa na ubalozi wa tanzania ulioko
Dubia,UAE kwmaba amepata kazi nchini humo,wakala wa huduma za ajira tanzania
umeridhia utaratibu uliotumika kwa kumuunganisha mtajwa hapo juu na fursa
ya ajira",inasema barua ya TaESA.
Barua hiyo iliyotumwa
uhamiaji kwa taratibu zadi ya kiuhamiaji,ilisainiwa na K.V.Kilindu
februari 12 mwaka huu kwa niaba ya mtendaji mkuu wa TaESA huku ikiwa
imebandikwa picha ya mwanaisha.
kwa mujibu wa mkataba
ambao nakala yake tunayo,mwanaisha alikuwa alipwe mshahara wa AED 1100
sawa na sh,460,000 za tanzania lakini kwa mujibu wa maelezo yake,alielezwa kuwa
atalipwa AED 800 sawa na sh,360,000 ambazo hata hivyo alidai hajawahi kulipwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni