U
|
salama wa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha ualimu cha Northern
Highlands Teachers College mjini Moshi upo mashakani kutokana na hofu ya
kuangukiwa na miti iliyoshikizwa katika jengo hilo .
Muonekano wa jengo la chuo
cha ualimu cha Northern Highlands mjini Moshi, upande wa mbele
Wakizungumza, wanafunzi hao bila kutaja majina yao, wamedai kuwa, hofu
ya usalama wao inatokana na ukweli kwamba,licha ya jengo hilo kutokamilika kwa
aslimia 100, hadi sasa ndilo linalotumika kama madarasa na hapo hapo linatumika
kwa ajili ya makazi yao.
Wamedai kuwa, Novemba 22 mwaka huu wanafunzi sita walilazwa katika
Hospital binafsi ya Kilimanjaro iliyopo mjini hapa baada ya kupata mshituko
uliotokana na kuanguka kwa moja ya tofari lililokuwa juu ya jengo hilo na
hivyo kuibua taharuki iliyosababisha wenzao kulazwa kwa siku mbili kwa
matibabu.
Hata hivyo,katika kuficha ukweli,mmoja wa wakurugenzi wa Bodi ya
chuo hicho, Henry Mallya, alikana kata kata kuwepo kwa tukio hilo ikiwamo
wanafunzi hao kulazwa hospitalini lakini baada ya waandishi kuanza kupiga picha
za jengo la chuo hicho,alianza kuwapigia simu na kuwasihi wasitoe habari za
tukio hilo.
Mallya alikutana na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki ofisini
kwake iliyopo shule ya sekondari ya Norther Highlands ambako alikana kuwapo kwa
tukio hilo, lakini baada ya nusu saa Mallya huyo huyo aliwapigia simu tena
waandishi wa habari akiwasihi wasichapishe picha za jengo la chuo hicho baada
yak upewa taarifa za wasaidizi wake juu ya picha hizo kupigwa.
Kwa mara ya pili Mkurugenzi huyo ambaye pia anamiliki shule
ya msingi ya The Moshi Academy, aliwaita waandishi wa habari kwenye ofisi yake
iliyopo kwenye majengo ya shule hiyo ya msingi na kuwasihi wasichapishe habari
au picha za chuo hicho akihofia ushindani wa kibiashara na licha ya kuelezwa
kuwa waandishi wa habari hawafanyi biashara, alisisitiza kutochapishwa kwa
habari hizi.
pole sana wanaosoma hapo na kweli ni hatari kwa usalama jitihada za maksudi zifanyike kabla ya madhara
JibuFuta