M
|
wanafunzi
wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari majengo,Said Seleman (14) mkazi
wa mtaa wa Arabika kata ya Majengo Manispaa ya Moshi, ametoweka nyumbani kwao
kwa zaidi ya miezi miwili sasa huku familia yake ikipoteza matumaini ya kumpata
kutokana na kutoonekana kila kona wanayomsaka.
Kwa
mujibu wa mama mzazi wa mwanafunzi huyo,salama saidi,kijana huyo alitoroka
nyumbani kwao Oktoba nane mwaka huu wakati mama yake akijiandaa kwenda na
mwanafunzi huyo shuleni kwao kutokana na kutuhumiwa kutenda utovu wa nidhamu.
Akizungumza
na blog hii, mama huyo alisema tangu siku hiyo wamekuwa katika harakati za
kumtafuta mwanaye bila kafanikio na kuomba watu wenye mapenzi mema ambao
watafanikiwa kumuona mwanaye watoe taarifa kituo chochote cha polisi au wampige
simu yake ya kiganjani namba 0754 03 63 12.
Kwa
mujibu wa mama mzazi wa mwanafunzi huyo, mwanaye alikuwa akituhumiwa
kujihusisha na wizi wa mabegi ya wanafunzi wenzake na kwenda kuyauza na kisha
kugawana fedha na wanafunzi wenzake na baada ya arobaini yake kufika siri
ikafichuka na kubanwa ili ataje washirika wake.
Pia
alisema, sakata hili lilifikishwa nyumbani kwao na mama huyo akashauri
likazungumzwe kwa uwazi shuleni na ndipo kijana huyo alioingiwa na hofu na
kisha kutimka kutokana na kuonywa na wenzake kuwa akikamatwa ni marufuku kuwataja
washirika wake.
Tayari
mama huyo ametoa taarifa za kupotelewa na mwanaye katika kituo cha polisi
majengo ambako jarada limefunguliwa na kupewa namba MAJ/RB/3513/2014.
Hima
hima wananchi kwa atakayemuona mwanafunzi huyo atoe taarifa zitakazosaidi
kupatikana kwake kwani kwa kitendo chake cha kutoroka nyumbani amekosa fursa ya
kufanya mtihani wa kidato cha kwanza na hivyo kuwa katika hatari ya kukosa
nafasi ya kusonga mbele kwa kidato cha pili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni