Mlima
Kilimanjaro (Tanzania) una vilele vitatu, Kibo, Mawenzi na Shira. Mlima huu
umepewa heshima na kuingizwa katika maajabu saba hapa ulimwenguni hasa
ikizingatiwa ni mlima uliosimama pekee yake bila kuungwa kwenye safu za milima
kama ilivyo Everest (Asia) kwenye mapangano ya milima ya Himalaya, Drakensburg
kwenye safu za milima ya Drakensburg (Afrika Kusini).
Mabalozi
wakiwa katika Mwamba wa Pundamilia “Zebra Rock” katika safari ya kuelekea
Kilele cha Uhuru (Uhuru Peak).
(Picha zote na
Charles Ndagulla)
Mlima
huu una urefu wa meta 5,895 sawa na futi 19,341 kutoka usawa wa bahari (a.s.l).
Ndagulla
Blog inaufunga mwaka 2014 ikiwa na rekodi ya kuupanda mlima huo.
Tukio
hili la kuupanda mlima lilianza Desemba 16 hadi 21 kupitia geti la Marangu hadi
kilele cha Uhuru (Uhuru Peak).
Mandhari
nzuri katika safari hiyo kunadhihirisha na namna gani mlima huu ulistahili
kupewa heshima.
Katika
safari hiyo Ndagulla blog iliongoza na Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi akiwemo
Batlida Buriani anayeiwakilisha Tanzania nchini Kenya.
Balozi
Lazia Msuya, anayeiwakilisha Tanzania huko Bondeni kwa Madiba alikuwepo katika
safari hiyo ngumu.
Mabalozi
wengine
Na.
|
Jina la Balozi
|
Nchi anayowakilisha
|
1
|
Dkt. Batlida Buriani
|
Kenya
|
2
|
Radhia Msuya
|
Afrika Kusini & Swaziland
|
3
|
Adadi Rajabu
|
Zimbabwe &
Maritius
|
4
|
Dkt. Ladislaus Komba
|
Uganda
|
5
|
Mbarouk N. Mbarouk
|
UAE
|
6
|
Dkt. Aziz P. Mlima
|
Malaysia
|
7
|
Dkt. Bernard Achilwa
|
|
8
|
Shamimu Nyanduga
|
Msumbiji & Madagascar
|
9
|
Grace Mwijuma
|
Zambia
|
10
|
Patrick TSere
|
Malawi
|
11
|
Ramadhan Mwinyi
|
UN
|
12
|
Mbelwa Kairuki
|
Mkurugenzi wa Asia
|
13
|
Celestine Mushi
|
Mkurugenzi
Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya nje
|
14
|
Daniel Ole Njoolay
|
Nigeria
|
15
|
Joseph Sokoine
|
Mkurugenzi Idara ya
Amerika na Ulaya
|
16
|
John Kijazi
|
|
17
|
Charles A. Sanga
|
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii
|
Hebu Tazama mtiririko mzima wa
safari hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na
mabalozi kabla ya kuwakabidhi bendera ya taifa la Tanzania katika safari
kuelekea kilele cha Uhuru (Uhuru Peak).
Safari
hiyo iliratibiwa na TANAPA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni