M
|
walimu wa Chuo cha Madrasa kilichopo Chake Chake, Pemba, Said
Khamis Salum (31) ameanza kutumikia chuo cha mafunzo jela miaka 7 baada ya
kutiwa hatiani kwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 15 jina
(linahifadhiwa).
Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ali Bilali aliiambia Mahakama ya Chake Chake mbele ya hakimu, Khamis Ramadhan Abdalla kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo miezi mitatu iliyopita .

Bilali alisema mashahidi watano waliitwa mbele ya Mahakama na
kukiri kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo. Alisema baada ya uchunguzi wa
vinasaba ( DNA), uliofanywa Tanzania Bara ulionesha kwamba kwa asilimia 96
mtuhumiwa ndiye aliyempa ujauzito mwanafunzi huyo.
Hakimu Abdalla alisema ameridhishwa na ushahidi wote, ikiwemo
ule wa kitaalamu wa vinasaba wa DNA, uliofanywa na wataalamu kutoka Tanzania
Bara, unaoonesha kwamba ni kweli mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Alisema mtuhumiwa atatumikia chuo cha mafunzo jela miaka saba,
na atakapotoka atalazimika kulipa fidia ya sh.milioni moja ikiwa ni fundisho
kwa wengine kuacha kufanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa wanafunzi wa vyuo
vya madrasa.
“Nimeridhishwa na mazingira ya makosa haya kwa mtuhumiwa na
kubaini kwamba ni kweli amempa ujauzito mwanafunzi wake wa chuo, kitendo
ambacho ni kinyume na sheria za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,” alisema
Adalla.
Mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea, alikana kosa hilo na
kusema anahisi kwamba alipitiwa na kurubuniwa na adui shetani, ambaye ndiye
aliyemshawishi kufanya hivyo.
Hivi karibuni, akizindua kampeni ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein alikemea tabia ya baadhi ya walimu wa vyuo vya madrasa kuwafanyia ukatili wa kijinsia wanafunzi wao na wengine kuwapa ujauzito.

CHANZO: HABARILEO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni