Kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi iliyowasilishwa katika
mkutano mkuu wa 20 wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika hivi karibuni mjini
hapa inaonyesha kuwa,kwa sasa benki hiyo ina mtaji wa sh,Milioni
195,111,000 tu hali ambayo wakaguzi hao wameonya kuwa inaweza kuathiri uwepo wa
benki hiyo.
Aidha taarifa hiyo imeonya kuwa,mikopo inayotolewa kwa
wateja imekuwa hairejeshwi kila mwezi kwa mujibu wa mikataba
iliyowekwa hali iliyopelekea kufutwa kwa mikopo mibaya yenye thamani ya sh,Milioni
255,611,441 kwenye vitabu baada ya kupata kibali kutoka bodi ya uongozi.
Wakati kiasi hicho kikubwa cha fedha kikufutwa,benki
hiyo ilifanikiwa kukusanya kiasi kidogo cha fedha cha sh,Milioni 62.073,000
huku taarifa hiyo ya ukaguzi ikigundua kuwapo kwa tengo la ziada la mikopo
mibaya la sh,33,740,683 likipitishwa kwenye
vitabu.
Taarifa hiyo ya ukaguzi imeendelea kufichua
kuwa,kuongezeka kwa matumizi yasiyo na riba kunachangia benki kutokuendelea
vizuri na kusababisha hasara ya sh,milioni 343,260,000 katika mwaka husika na
kuongeza jumla ya hasara kutoka sh,Bilioni 1.169,834,000
mwaka 2012 hadi sh,Bilioni 1.513,094,000 mwaka jana.
Hata hivyo menejimenti ya benki hiyo imejibu hoja hizo
za ukaguzi na kuelezea kuwa itaongeza biashara kwa sh,Bilioni 1.5 ambayo
itazalisha mapato ya sh,Milioni 150 ili kuongeza faida bila kuonyesha
mchanganuo jinsi itakavyoongeza biashara hiyo.
Katika hatua nyingine,benki hiyo inakabiliwa na changamoto
kubwa ya kuhakikisha inarejesha mabilioni ya shilingi yaliyotolewa na benki
hiyo kwa wateja mbalimbali kama mikopo kutokana na kuwapo na mwitikio mdogo
katika ujereshaji
wake.
Taarifa ya meneja wa benki hiyo,Elizabert Makwabe kwa
mkutano mkuu wa wanahisa hao imeeleza kuwa,hadi kufikia septemba 30 mwaka huu
jumla ya sh,Bilioni 4.333,036,114 zilikuwa zimetolewa kama mikopo kwa wateja
mbalimbali.
Inaeleza kuwa aslimia 63.3 ya mikopo hiyo ilielekezwa
katika sekta ya kilimo ambayo ni kiasi cha sh,Bilioni 2.758,217,111 na kwamba
ni sh,Milioni 370,258,855 tu zilizokuwa zimekusanywa katika kipindi cha kuanzia
januari hadi septemba mwaka huu.
Meneja huyo amelalamika kuwa,baadhi ya wateja wanatumia
njia mbalimbali ili wachelewe kulipa na wakati mwingine wanatumia kauli za
matusi pale inapolazimika madeni yasiyolipwa yakusanywe.
Alitoa wito kwa wale wote ambao hawajarejesha au
marejesho yao hayaendi vizuri,kuchukua hatua za makusudi na kulipa madeni yao
na kwamba bila kufanya hivyo benki italazimika kutenga matengo kwa ajili ya
madeni mabaya hali itakayoathiri mtaji wa benki hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni