Jumatano, 24 Desemba 2014

TALAKA YAMFANYA BISHOP MOLLA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA



Askofu Mkuu wa Kanisa la Furaha hapa nchini (KLFT) Jones Molla amefunga pingu za maisha baada ya mahakama kutoa talaka ya mke wake wa kwanza waliyefunga naye ndoa mwaka 1978.

 Bi. JACKLINE SHUMA NA ASKOFU JONES MOLLA BAADA YA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA


Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa la Biblia, lililopo Pasua mjini Moshi Jumapili iliyopita huku mamia ya waumini wa makanisa hayo wakishuhudia tukio hilo ambalo Askofu Molla alifunga pingu za maisha na Bi. Jackline Shuma.

Itakumbukwa kwamba Mahakama ilitoa talaka ya kufikia ukomo wa ndoa ya Askofu Molla mwezi Julai mwaka huu kwa mke wake wa kwanza Lilian Kimambo waliyezaa naye watoto 10 wakifunga pingu za maisha mwaka 1978.

Misukosuko ya ndoa ya Askofu huyo iliingia doa mwaka 1993 ambapo ilifikia hatua ya kupelekana mahakama ilikofikia ukomo na mahakama ya mwanzo mjini Moshi mwaka huu ikihitimisha sakata hilo lililochukua zaidi ya 20.

Kwa upande wake Askofu Molla alisema kuwa ameachana na mkewe huyo kutokana na fitina alizokuwa akizipokea kutoka kwa baadhi ya wachungaji wa kanisa la kipentekoste.

Tangu mwaka 2009, mke aliondoka nyumbani na kwenda kuishi na wazazi wake, kinyume na maandiko ya Mungu ambayo yanasema utaambatana na mume wako hadi kifo kitakapo watenganisha.

Hatua ya Mahakama kuvunja ndoa hiyo ilitolewa na shauri la talaka lililofunguliwa katika mahakama hiyo na Askofu Molla Na.  16/4/13 akidai tangu mwaka 2009 mkewe Lilian alitoroka nyumbani na juhudi za kumrejesha zimekwama.

Aidha Mchungaji kiongozi wa kanisa la kipentekoste Majengo, James Rukate amekiri kanisa lake kufungisha ndoa hiyo mwaka 1978, na kuwa walipewa shahada No 42335 na kuwa shahada hiyo imeonyesha kuwa wakati huo wawili hao walikuwa watu wazima miaka 30 kila mmoja , na walishaanza  kuishi pamoja.

Ndoa hiyo ilifungishwa na Mchungaji    Japhet Mark Kyara kutoka Dar es Salaam ambaye ni msajili wa ndoa anayetambulika na sheria wa masuala hayo ya mwaka 1971 na kuongeza kwamba hakuna kikwazo chochote baada ya tamko la mahakama kuwa ndoa ya Askofu Molla ni halali.

Wanandoa wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kufunga pingu za maisha walisema Mungu amewapigania kutokana na hali ya utata iliyokuwepo katika sakata hilo gumu na wataendelea mbele kumtumikia Mungu.

Pande zote mbili za mke na mume ziliridhia ufungwaji wa ndoa hiyo.

CHANZO: JAIZMELALEO / MCRCTV

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni