Ijumaa, 12 Desemba 2014

KUBADILISHA VIWANGO VYA UFAULU MARA KWA MARA, CHANZO CHA KUDIDIMIZA ELIMU



W
adau wa elimu nchini   wameishutumu serikali  kwa kubadilisha mara kwa mara viwango vya ufaulu bila kufanya tathmini ya kutosha mpango uliofananishwa na upanuzi wa magoli ili kumwezesha kila mchezaji kufunga kirahisi.

Shutuma hizo zilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa shule ya sekondari Majengo iliyopo chini ya kanisa Katoliki Jimbo la Moshi,Peter Lyimo katika hotuba yake kwenye mahafali ya 28 ya wahitimu 568 wa kidato cha nne .

Br.Peter Lyimo
Mwalimu mkuu  wa shule ya sekondari Majengo
Alisema kuwa hali hiyo ni ya hatari na kmwaba inaua elimu na taifa haliwezi kuendelea kwas mfumo huo na kushauri serikali kuiboresha elimu ili iweze kuandaa wanafunzi kuweza kujitegemea .

Aliitaka serikali kuziboresha shule za ufundi na kuzipa msukumo wa pekee akiamini kuwa ni mhimu sana kwani zinawezesha kuzalisha kazi badala ya kufatufa kazi.

Mkuu huyo wa sekondari majengo alisema kuwa,elimu ya tanzania  haiwezi kuwa bora kama wananchi hawataimiliki  kwa mchango na uwajibikaji na kuongezak uwa kama taifa na jamii yanahitajika mabadiliko ya kifikra  na kimtazamo kuhusu elimu .

“Ndugu zangu,tunatakiwa kuchangia elimu yetu ili iwe bora ,kuna wanafanzi wengi ambao wanashindwa kusoma kutokana na kukosa msaada tunakumbuka kwamba kila mmoja wetu hapa amefika alipo kwa kutembea mgongoni mwa mtu mwingine,baba,mama,mjomba,shangazi,ndugu n.k”alisema.

Alisema pamoja na  kubadili viwango vya ufaulu na kuwa na daraja la tano, bado tatizo la ajira lipo palepale na zaidi ya yote linazidi kuwa kubwa zaidi kutokana na wengi wa wanaohitimu vyuo vikuu kutokuwa na ujuzi na kuongeza kuwa endapo shule za ufundi zingepewa kipaumbele tatizo hilo lingepungua .

Alionya kuwa kwa kutopewa kipaumbele elimu ya ufundi  ni mzigo ambao serikali inajitakia kwani endapo ingetilia mkazo  elimu hiyo ,kila mhitimu anayehitimu chuo kikuu angeweza kuwa na ujuzi na kujiajiri wenyewe  badala ya kusubiri kuajiriwa.

Aidha Lyimo aliiasa jamii kubadilika  kifikra kwa kuwekeza katika elimu badala ya kuwekeza kwenye harusi jambo ambalo haliisaidii jamii na badala yake elimu inazidi kushuka siku hadi siku na kupelekea tatizo la ajira kuzidi kuwa kubwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni