Walimu
wakuu 16 wa shule za msingi mkoani Dodoma wameshushwa vyeo baada ya kushindwa kuwajibika
vyema.
Ofisa
elimu wa mkoa, Juma Kaponda alisema hayo katika mkutano wa wadau wa elimu
ulioandaliwa kwa ajili ya kutangaza matokeo ya darasa la saba.
Kaponda
alisema walimu hao wakuu wanatoka katika shule za Mwiyendaje na Segara wilayani
Chamwino na wengine wanane wanatoka wilayani Chemba.
Walimu
wakuu wengine waliokumbwa na kadhia hiyo ni wa shule za Kongogo, Mkakatika na
Bankororo wilayani Bahi.
Katika
Wilaya ya Mpwapwa walioshushwa vyeo ni walimu wakuu wa shule za Luhundiwa na
Idiro.
Kaponda
alisema Dodoma ilishika nafasi ya 21 kitaifa katika matokeo ya mtihani wa
darasa la saba mwaka huu, wakati mwaka jana ulishika nafasi ya 23.
Hata
hivyo, alisema takwimu zinaonyesha kuwa kiwango cha ufaulu kwa mwaka jana
kilikuwa ni asilimia 38.2 (sawa na wanafunzi 15,053) na mwaka huu kimepanda na
kufikia asilimia 45.3 (sawa na wanafunzi 16,672)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni