Z
|
aidi ya wananchi 1000 wanaoishi kuzunguka msitu wa
asili wa Bombo makole uliopo wilayani hapa wapo hatarini kukosa maji
kutokana na tishio la kukauka kwa vyanzo vya maji vinavyotiririsha maji
kwa wananchi hao kutoka katika msitu huo.
Tishio hilo la kukauka kwa vyanzo vya maji linatokana na kasi ya
uvunaji haramu wa mbao kutoka katika msitu huo unaofanywa na
wafanyabiashara kwa kushirikiana na maofisa misitu wasio waaminifu wanaodaiwa
kutoa vibali vya kuvuna magogo katika msitu huo kwa kisingizio cha shughuli za
maendeleoe.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi kwa zaidi
ya wiki mbili wilayani hapa,umebaini kuwa,halmashauri ya wilaya ya Lushoto
kupitia amati ya uvunaji imekuwa ikitumia mwanya huo kushirikiana na
wafanyabiashara uhumu msitu huo.
Msitu huo ambao upo chini ya Halmashauri ya wilaya ya Lushoto
umekuwa kichocheo kikubwa cha upatikanaji wa maji kutokana na kusheheni miti ya
asili inayowezesha upatikanaji wa maji kwa mwaka mzima .
Akizungumza, mwenyekiti wa kijiji cha makole kilichopo kata ya
Kilole,Athuman Tupa,alisema kuwa kama hatua madhubuti hazitachukuliwa uuokoa
msitu huo,wananchi wa vijiji hivyo wataathirika kwa kiwango kikubwa na ukosefu
wa maji.
Alisema kuwa,licha ya halmashauri ya wilaya ya Lushoto
kuwachagisha fedha wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule,wananchi wa maeneo
hayo hawanufaiki na raslimali za msitu huo kutokana na kuwanufaisha watu
waliopo nje ya eneo lao.
Naye diwani wa kata ya Kilole,Salehe Manyenya,alisema kuwa pamoja na
uvunaji huo wa magogo kuendelea,shule nane za msingi zilizopo kuzunguka msitu
huo,zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati licha ya halmashauri ya wilaya
kudai kuwa magog hayo yanavunwa kwa ajili ya matengenezo ya madawati.
Alizitaja shule hizo kuwa ni MziMkuu, Kwekanga, Makole, Ngwelo, Kwemanoo,
Hemtoye, Chaumba ba Kwedeghe ambazo baadhi ya wanafunzi wamekauwa wakisoma huku
wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba huo wa madawati.
Hata hivyo ofisa msitu wilaya ya Lushoto,Rashirid Hassan alikataa
kuzugumzia shutuma hizo kwak ile alichodai yeye si msemaji wa halmashauri licha
ya nyaraka kuonyeshe kuwa yeye ndiye mmoja wa maofisa wa idara ya misitu ambao
wamekuwa wakitoa vibali vya ununaji wa magogo.
Kwa
mujibu wa nyaraka ambazo mwandishi anazo,desemba 2 mwaka jana ofisa misiti huyo
alitoa vibali viwili kwa watu waliotajwa kwa majina ya Kumbula
Mbangula na Bebwa G.Ludovick kwa ajili ya uvunaji wa aina ya mikaratusi vibali
ambavyo wananchi hao wanadai kuwa vinatumika kwa ajili ya kukata miti ya asili
na si mikaratusi.
Hata hivyo vibali hivyo vinaonyesha waliopewa wanaruhusiwa kukata
miti kwa ajili ya shughuli za maenndeleo na shughuli binafsi vibali ambavyo
havifafanui shughuli binafsi ni zipi na shughuli za maendeleo ni zipi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni