Mshambuliaji
wa zamani wa Ufaransa Thierry Henry amestaafu kandanda la kulipwa baada ya
miongo miwili na sasa atakuwa mchambuzi wa kandanda kwenye televisheni ya Sky
Sports nchini Uingereza.
Henry
(Anri) mwenye umri wa miaka 37, alishinda Kombe la dunia na la Ulaya akiichezea
timu ya taifa ya Ufaransa, na pia ndiye mfungaji wa magoli mengi zaidi katika
klabu ya Arsenal kwenye Ligi Kuu ya England akiwa na mabao 226 katika mechi
370.
Kocha
wa Arsenal Arsene Wenger alisema hivi karibuni kuwa Henry "bila
shaka" atajiunga tena na klabu hiyo katika wadhifa mwingine katika
siku za usoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni