Arusha Serena Hotel,Resort and Spa
NA CHARLES NDAGULLA,ARUSHA
RUSHWA ya ngono ni moja ya vitendo ambavyo vimekuwa
vikiwakwaza wanawake katika kupata ajira
maeneo mbali mbali duniani hatua ambayo inatajwa kama moja ya changamoto kubwa
katika mafanikio yao.
Kutokana na
kukithiri kwa vitendo hivyo,wapo baadhi yao ambao licha ya kuwa na sifa za
kuajiliwa wamejikutaka wakikosa fursa hizo kutokana na kushindwa kutoa rushwa
ya ngono kwa wanaosimamia mamlaka za ajira.
Pamoja
na kelele ninyi kupigwa kutoka kwa
watetezi wa haki za binadamu yakiwamo mashirika yasiyo ya kiserikali juu ya kukithiri kwa vitendo hivyo,mambo bado
yahajabadilika katika baadhi ya maeneo ya kazi hapa nchini.
Wafanyakazi
wa kike katika Hotel ya kitalii ya Arusha Serena Hotel and Resort iliyopo
kilometa 4.5 kutoka eneo la Tengeru nje ya Jiji la Arusha ni moja ya wahanga wa
matukio hayo ya unyanyasaji wa kingono.
Wafanyakazi
hao walioomba kutotajwa majina yao kwa sababu maalumu,wamezungumza na waandishi
wa habari Jijini Arusha na kuelezea kilio chao juu ya vitendo hivyo ambavyo
wanadai vinawakwaza katika utendaji kazi wao.
Kwa mujibu
wa wafanyakazi hao,wamedai wengi wa wanaonyanyasika ni wafanyakazi wa
kitanzania huku wafanyakazi kutoka nchini Kenya wakipewa huduma nzuri ikiwamo
mishahara minono na maslahi mengine.
Ndagullablog imezungumza na meneja Raslimali watu
wa hotel hiyo John mwamakula juu ya malalamiko ya wafanyakazi hao kunyanyaswa
kingono na baadhi ya maofisa wa hotel hiyo akiwamo meneja wake Filex Ongembo.
Katika
mahojiano na Ndagullablog ofisini
kwake wiki hii,Mwamakula hakukiri wala kukanusha malalamiko hayo huku
akisisitiza vitendo hivyo ni kinyume na sera ya hotel hizo.
Amesema sera
ya hotel hizo zilizopo maeneo mbali mbali nchini inakataza vitendo hivyo na
kwamba anayebainika kufanya hivyo anakuwa katika hatari ya kufukuzwa kazi.
Mwamakula
amesema kuwa hawajawahi kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao
kunyanyaswa kingoni lakini akadai zipo njia tatu kwa wafanyakazi hao
kuwasilisha malalamiko yao kwa uongozi.
Ametaja njia
hizo kuwa ni pamoja na utoaji taarifa kwa njia ya siri(wisow blower),mfanyakazi
kwenda moja kwa moja ofisini kwake na kupitia mikutano ya wafanyakazi(Staff
General Meeting) ambayo amedai hufanyika kila baada ya miezi mitatu.
“Kwa ujumla
hatukubaliani na hivyo vitendo na hata ukiangalia sera yetu inakataza vitendo
hivyo na adhabu yake ni kali sana kama ikibainika mtu amehusika na vitendo
hivyo tunamfukuza kazi”,amesema.
Hata hivyo
meneja huyo alipoulizwa alipo Ongembo amesema hajui alipo zaidi ya kusema
hayupo na taarifa ambazo jamhuri limezipata ni kwamba meneja huyo amerejeshwa
nchini kwao Kenya.
Malalamiko
mengine ya wafanyakazi hao ni kupunguzwa kwa mishahara yao kwa aslimia tano
tangu mwaka jana na meneja huyo amekiri kuwepo na punguzo hilo la mishahara kwa
wafanyakazi hao.
Akijibu
malalamiko hayo,Mwamakula amesema kuwa,makato hayo yalitokana na kuyumba kwa
biashara ya utalii mwaka jana madai ambayo wafanyakazi hayo wameyapinga.
Huduma ya matibabu ni moja ya malalamiko mengine
kwa watumishi ambako wanadai mwajili wao kuwaondoa kwenye huduma ya matibabu
kupitia bima ya Afya(NHIF) huku wakitibiwa kupitia bima ya Jubilee ambayo
wamedai haiwapi nafasi ya kwenda kutibiwa katika hospital za rufaa.
Wametaja
changamoto nyingine kuwa ni pamoja na kutopewa usafiri wa kutoka nyumbani
kwenda kazini na kurudi majumbani hali ambayo imewalazimu kutumia zaidi ya
shilingi 10,000 kwa siku kama gharama za usafiri fedha ambazo wanadai
zinazotoka kwenye sehemu ya mishahara yao.
Licha ya kutopewa
usafiri,wafanyakazi hao wamedai kuwa usalama wao uko shakani kutokana na
kutumia usafiri wa boda boda usiku wa manane wakati wa kutoka kazini kutokana
na boda boda wengi kutowafahamu.
“Tunaomba
mtusaidie kwa kweli hali ni mbaya,wafanyakazi wa kitanzania tunanyanyasika sana
tofauti na wenzetu wakenya ambao wanaishi vizuri licha ya baadhi yao kutokuwa
na hadhi ya kufanyakazi ambazo tunauwezo nazo”,wamesema.
Hata hivyo
wafanyakazi hao wamedai kuwa,wamekuwa
katika tishio la kufukuzwa kazi pindi wanapodai kuboreshewa mazingira ya kazi
hatua ambayo imewafanya baadhi yao kukaa kimya kwa hofu ya kufukuzwa kazi.
Wafanyakazi
hao wameitaka wizara ya kazi,ajira na vijana
pamoja na idara ya uhamiaji Jijini Arusha kufanya uchunguzi wa kina kwa
baadhi ya wafanyakazi wa hotel hiyo kutoka nchini Kenya kwani baadhi yao hawana
sifa za kufanyakazi hapa nchini.
“Ukienda
pale ofisi kuu utawakuta wakenya wamejazana pale wengine hawana sifa za kuwa
hapa nchini kwa sababu baadhi ya kazi wanazofanya hazihitaji watu kutoka nje ya
nchi,wapo wanafanyakazi kama makatibu mhitasi,je kazi hiyo inahitaji mtu kutoka
Kenya?,wamehoji.
Kuhusu suala la matibabu,Mwamakula amesema
kuwa si kweli bima ya Jubilee inawanyima fursa ya kutibiwa katika Hospital za
rufaa huku akikiri kujiondoa katika Bima ya Afya ya NHIF.
“Mpango wetu
wa matibabu unagusa mfanyakazi na mwenza wake kama ameoa ama kuolewa na watoto
wasiozidi wanne wenye umri chini ya miaka 18”,amesema.
Amesema
wafanyakazi hao pia ni wanachama wa mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) ambako
kuna mpango wa matibabu kupitia fao la
matibabu ambako mwanachama anaweza kujiandikisha bila kuathiri michango yake na
akachagua Hosptil anayoitaka.
Mbali na
huduma hizo,meneja huyo amesema wafanyakazi hao wanayo bima nyingine ambako
matibabu yakishindikana hapa nchini wanaweza kupelekewa nchini Kenya kwa
matibabu zaidi.
Jamani wakenya wameshatuchosha kabisa sio hata Serena tu, mahotel mengi watanzani wamekuwa wakionwa kama mambwa mwitu ndugu zangu. Wamekuwa wakilipwa mishahara mingi lakini watenda kazi walio wengi ni watanzania, ukilinganisha mshahara Wa mtanzania hata robot ya mahitaji yake ya mwezi haufiki, as kama watanzania tu naomba sana haya mashirika ya kazi yatembelee hizi hotel, tunateseka jamani watu hawana overtime wala nn
JibuFutaMarandu nakushukuru kwa maoni yako,tunajipanga kuwasiliana na waziri mwenye dhamana na ajira tumfikishie hayo malalamiko,yapo mengi sana kwa kweli na kama ulivyosema si serena pekee,hivyo tukimpata waziri mwenye dhamana tutafanya naye mahojiano na kupata msimamo wa serikali,naomba nikutakie siku njema na uendelee kutembelea blog yetu na usisite kutoa maoni yako.
JibuFutaSafi sana Ndagulla keep it up.
JibuFutaThanks For Information.
JibuFutaBest Hotels in Arusha
http://www.crestsafarilodge.com/
Crest Safari Lodge is the perfect choice, if you are in search of Budget Hotels. Crest Safari Lodge is one of the Best Hotels in Arusha, just right for Camping and Cultural Tours.