Alhamisi, 6 Novemba 2014

UVAMIZI MAPITO YA WANYAMA HIFADHI YA TARANGIRE, WATISHIA UHAI WA WANYAMA



H
ifadhi  ya Taifa ya Tarangire ilianzishwa mwaka 1970 kwa tangazo la serikali namba 160 lengo likiwa ni kuhifadhi makimbilio ya wanyama wakati wa majira ya kiangazi.
 
Malengo mengine ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo ni kuhifadhi maeneeo ya mto Tarangire unaobeba jina la hifadhi hiyo pamoja na ardhi oevu ambayo ni chanzo pekee cha maji wakati wa majira ya kiangazi.

Inaaminika kwamba,kipindi hicho cha kiangazi ndicho kipindi ambacho wanyama kunakuwapo na mkusanyiko mkubwa wa wanyama katika eneo la hifadhi.

Wanyama hao  huhama ndnai ya hifadhi hiyo kuelekea masahriki,kaskazini na kusini kwa ajili ya malisho na kuzaliana hususani wanyama kama nyumbu na pundamilia katika miezi ya Oktoba na Novemba ambayo ni kipindi cha masika.

Pamoja na umhimu wa hifadhi hiyo kuichumi kutokana na kuwa moja ya hifadhi tano zinazozalisha ziada,kumekuwapo na changamoto nyingi zinazochanhgia kukwaza shughuli za uhifadhi.

Mkuu wa hifadhi hiyo(CPW),Stephano Qolli,anasema moja ya changamoto zinazokwaza shughuli za uhifadhi ni tishio la kutoweka kwa wanyama kutokana na kuvamiwa kwa mapito yao kutokana na shughuli za kibinadamu.

Anasema kasi ya ongezeko la idadi ya watu na matumizi ya ardhi litaifanya hifadhi hiyo kuwa kisiwa  endapo hatua za makusudi hazitachukuliwa katika kuyalinda mapito hayo ya wanyama.

Katika taarifa yake kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,maliasili na mazingira,Mkuu huyo wa hifadhi anasema kuwa,kuna hatari hifadhi hiyo ikatenganishwa na maeneo ya mazalio ya wanyama na mlisho.

Alionya kuwa,wanyama hao wanaweza wakapungua ama kutoweka kabisa endapo maeneo hayo ya malisho yataharibiwa  kutokana na ongezeko kubwa la shughuli za kibinadamu.

Aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa,katika kukabiliana na changamoto hizo,hifadhi imekuwa  ikitoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali pamoja na kusaidia mradi wa mpango wa mtumizi bora ya ardhi hususani katika vijiji jirani.

Tishio la kuharibiwa vyanzo vya mto Tarangire

Pamoja na tishio la kutoweka  kwa wanyam katika hifahdi hiyo kutokana na kuvamiwa kwa mapito yao,shughuli za kibinadamu ikiwamo kilimo,ufyekaji misitu na ufugaji vimedaiwa kuathiri vyanzo vya maji katika mto tarangire.

Kwa mujibu wa mhifadhi huyo,mto tarangire unaanzia katika milima ya kondoa takribani kilometa 50 kusini mwa hifadhi hiyo ambapo mbali na milima hiyo ya kondoa,pori la akiba la mkungunero nalo ni mojawapo ya chanzo.
Anasema pori hilo pamoja na sehemu ya kusini nalo limevamiwa na mifugo mingi huku shughuli kubwa za kilimo zikiendelea kwa kasi hali ambayo inaweza kuhatarisha uwepo wa hifadhi hiyo.

"tatizo hili linahitaji uelimishwaji wa jamii pamoja na utatuzi wa migogoro ya mipaka kati ya vijiji na maeneo yaliyohifadhiwa na kati ya mikoa ya dodoma na manyara",anasema.


Migogoro ya mipaka

Migogoro ya mipaka ndani ya hifadhi za taifa na misitu ya hifadhi ya taifa limekuwa ni tatizo sugu na ambalo kwa hakika bado halijapatiwa ufumbuzi wa kina na mamlaka husika.

Hali hiyo imeleta misuguano ya mara kwa mara baina ya ungozi wa hifadhi husika kwa upande mmoja na wananchi wanaoishi kuzunguka maeneo hayo ya hifadhi kwa upande wa pili.

Vivyo hivyo hifadhi ya taifa ya tarangire nayo hasijaachwa nyuma katika migogoro hiyo ambko mpaka sasa upo mgogoro unaofukuta katika kijii cha Kimotorok kinachopakana na hifadhi hiyo.

Kijiji hicho kipo wilaya ya Simanjiro lakini mpaka wa kijiji hicho umevuka mpaka wa wilaya na kuingia wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma hivyo utatuzi wake unahitaji ushirikiano wa mikoa hiyo miwili.

Kwa mujibu wa mhifadhi huyo,wananchi wa kijiji hicho hawautambui mpaka wa kijiji kama unavyoonekana katika ramani ya mwaka 1993 huku pia wakikataa kuutambua mpaka wa hifadhi baada ya kuhakikiwa mwaka 204.

Wananchi hao pia wanadaiwa kutolitambua pori la akiba la Mkungunero kwa madai kuwa hawakushirikishwa katika uanzishwaji wake na pia hawautambui mpaka uliopo kati ya mkoa wa Dodoma na Manyara.

Mhifadhi huyo anasema kuwa,endapo eneo hilo   litabaki kwa shughuli za kibinadamu,hifadhi ya tarangire na pori la akiba la Mkungunero zitakuwa
zimetenganishwa.

Anasema kuwa kutenganishwa huko kutaleta athari kubwa kimazingira na kiikolojia ikiwamo kufungwa kwa mapito ya wanyama ambako mapato yatokanayo ya utalii yatapungua.

Ametaja athari nyingine kuwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira utakaotokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu ikiwamo mifugo,kilimo na makazi hivyo kuathiri mtiririko wa mto Tarangire.

Ngoma ya asili  ikichezwa katika uzinduzi wa mradi wa wa majengo ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi ya Sangaiwe mkoani Manyara uliofanywa na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge,Ardhi,Maliasili na Mazingira,James Lembeli hivi karibuni

Imetayarishwa na:
Charles Ndagulla
+255-(0)-783 847 877

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni