Jumamosi, 11 Novemba 2017

UELEKEO MPYA MALIASILI NA UTALII- DKT.HAMISI KIGWANGALLA



KWA UFUPI: Uelekeo Mpya wa Maliasili na Utalii.
-------------------
Na Dkt. Hamisi Kigwangalla.


Tunajipanga kufanya makubwa yafuatayo:
Moja, kuongeza idadi ya wageni kuingia nchini kwa kufanya 'offensive marketing'. 

Tunaweka mikakati ya kuvutia zaidi watalii kutoka masoko mapya ya middle east (kipindi chao cha joto kali) na Far East (Tunaunda package maalum za kanda hizi).

Tutakuza idadi ya watalii wa ndani kwa kutumia mikakati mseto ya kutangaza utalii wa ndani na tunatengeneza 'package' rahisi ya watalii wa ndani kwa ajili ya kuvutia watalii wa ndani hususan kwenye vipindi vya 'low season'.

Pamoja na 'packaging strategy' yetu kulenga masoko fulani maalum, tunalenga kuitangaza zaidi nchi yetu kwenye 'travel expos' nyingi zaidi duniani (wiki hii nimetuma team yetu kwenye maonesho ya safari makubwa zaidi duniani yanayojulikana kama 'World Travel Market'.

Na wameambatana na Tour Operators kadhaa ambao watafanya mikutano ya 'networking' na wenzao wa masoko mengine duniani.

Pia tunalenga kutumia role models na hususan travel bloggers mashuhuri duniani kuja kutalii na kushuhudia vivutio vyetu kisha kuweka 'experience' zao kwa picha ama video kwenye 'social media accounts' zao.

We need more presence kwenye social networks ili kuvionesha vivutio vyetu na tutapenya kwenye masoko hayo niliyoyataja kwa kutumia watu mashuhuri wanaopatikana kwenye makundi haya ya masoko niliyoyataja.

Tutaendelea kuyalinda masoko yetu 'traditional' ya nchi za Ulaya na Marekani ya Kaskazini (defensive strategy) kwa mikakati hiyo hiyo.

Mbili, tunawekeza zaidi nguvu zetu kwenye kuongeza idadi ya siku ambazo watalii wanakaa nchini kwa kuongeza idadi ya vivutio na shughuli ambazo mtalii atafanya hapa nchini.

Tutawekeza nguvu zetu kwenye kuanzisha vivutio vya burudani na vya utamaduni. Tuko mbioni kuanzisha Dar Bus Tour, Arusha Bus Tour, Presidential Museum, Theme Park, Tanzania Heritage Month.

Tatu, tunaendelea kuhifadhi vivutio vyetu vya kipekee vya wanyamapori, uoto wa asili, mito, milima na fukwe, malikale na kuwekeza kwenye 'information centers' kwenye vivutio hivi. Pia kualika wawekezaji kujenga facilities kwa ajili ya wageni kwenye vivutio vipya na maeneo mapya ya kitalii.

Nne, tutawekeza kwa kushirikiana na taasisi nyingine, za umma na binafsi, kwenye utalii wa mikutano na Utalii wa matukio (michezo, mashindano nk). Malengo yakiwa ni kuvutia zaidi matukio ya kikanda na kimataifa kufanyikia nchini mwetu.

Tano, mambo mtambuka ya kimkakati tunayofanya ni pamoja na kwenda 'electronic' kwenye ukusanyaji mapato, huduma kwa watalii na usalama wa wanyamapori, usalama wa maeneo ya vivutio na usalama wa watalii wetu.

Kuunganisha uchumi wa watu wanaotuzunguka na shughuli za uhifadhi na Utalii kwa ujumla wake, na kuimarisha mnyororo mzima wa huduma za ukarimu nchini.

Mwisho, nimeagiza taasisi zote chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuwekeza kwenye mkakati huu wa 'diversification' ya vivutio na kuongeza idadi ya siku na kiasi cha fedha ambazo mtalii anatumia nchini kwetu.

 Aidha, vivutio vipya lazima viunganishwe na sakiti za sasa na mpya za utalii tunazozungumzia. Na ni lazima viwahusishe wananchi wa maeneo husika (linkage ya utalii na maisha ya wananchi).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni