RUNGU la mamlaka ya mapato
Tanzania(TRA) kufunga akaunti za walipakodi wakorofi na kukamata mali zao limeikumba Mamlaka ya Maji safi na maji taka Moshi Mjini(MUWSA) ambako akaunti za mamlaka hiyo
zinadaiwa kufungwa.
Kufungwa kwa akaunti za mamlaka hiyo
kulikodhibitishwa na mkurugenzi wake Joyce Msiru ni kutokana na madai
kwamba mamlaka hiyo inadaiwa shilingi Bilioni 2.6 ikiwani malimbikizo ya kodi
mbali mbali.
Hata hivyo mkurugenzi huyo wa
MUWSA Joyce Msiru anapinga deni hilo akidai baadhi ya kodi zilizoanishwa na TRA
hawawezi kuzilipa kutokana na wao(mamlaka) kutojiendesha kibiashara huku
akidaia TRA imesisitiza lazima madeni hayo yalipwe.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
TRA,kiasi hicho cha deni ni kutokana na ukaguzi uliafanywa kati ya mwaka 2013
hadi mwaka jana ambsalo linahusisha kodi mbali mbali ikiwmao VAT,Corporation
tax,Skillls Development Levy na nyinginezo.
Mkurugenzi huyo amesema mamlaka yake
haiwezi kulipa kodi ya Coporation tax inayofikia shilingi Milioni 847 kutokana
na kile alichodai mamlaka yake haifanyi biashara badala yake inategema mapato
kutokana na Ankara za maji kutoka kwa wateja.
“Mfano hiyo kodi ya coporation tax
wanayotudai hiyo ni kodi inayolipwa na makampuni au taasisi zinazojiendesha
kibiashara lakini sisi MUWSA income yetu inatokana na Ankara za maji
zinazolipwa na wateja,sasa hapo sisi tunahusikaje?”,alihoji.
Kuhusu shilingi Milioni 948
ambazo TRA inaidai MUWSA kama kodi ya ongezeko la thamani(VAT) mkurugenzi
hiyo amedai kuwa kuna mkanganyiko mkubwa katika kutafsiri sheria kutokana na
kwamba kwenye maji sheria imesamehe VAT lakini kwenye huduma ya majitaka sheria
imekaa kimya.
Kodi nyingine ambayo mamlaka hiyo
wanadai hawastahili kulipa na ambayo TRA wamesisitiza lazime ilipweni ya Skills
Development Levy ambako wanadaiwa shilingi milioni 569.
Akizungumzia kodi hiyo,mkurugenzi
huyo anadai kuwa mwaka 2012 TRA waliirejeshea mamlaka hiyo kiasi cha shilingi
milioni 39 baada ya kutozwa na mamlaka hiyo katika mwaka 1999 na 2002 na kuhoji
iweje kodi hiyo irejeshwe tena kwa mamlaka yake.
Kutokana na mvutano huo ,mkurugenzi
huyo amedai kuwa kwa sasa sakata hilo limepelekwa kwa katibu mkuu wa wizara ya
maji,profesa Kitila Mkumbo kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi huku taarifa
zikipasha kuwa sakata hilo sasa limeziunganisha wizara mbili,wizara ya maji na
wizara ya fedha.
Mbali na kupelekwa huko,mkurugenzi
huyo ameliambia Jamhuri kuwa imeundwa timu itakayoshughulikia madai ya
mamlaka za maji kote nchini ambako inadaiwa kuwa zimekuwa zikitozwa kodi na TRA
kadri wanavyoona.
“Lengo letu tunataka kuwe na mfumo
unaoeleweka wa utozwaji kodi kwa mamlaka zote nchini tofauti na sasa ambako
utasikia mamlaka hii wanatozwa kodi fulani,sasa huu mkanganyiko tunataka
tuumalize”,alisema.
Kutokana na kufungwa kwa akaunti za
mamlaka hiyo,wafanyakazi kadhaa wa mamlaka hiyo walijawa na hofu ya kukosa
mishahara yao ya mwezi oktoba lakini taarifa zilizopatikana baadaye na
kudhibitishwa na mkurugenzi huyo,TRA imeregeza kamba na kuzifungua huku
ikitishiak uzifunga tena kama hakitaeleweka.
WADAIWA SUGU MUWSA NAO KUKIONA CHA MOTO
Wakati Mamlaka hiyo ikitikiswa kwa
akaunti zake kufungwa na TRA na baadaye kufunguliwa kwa masharti,mkurugenzi
huyo amesema kuwa,mamlaka yake bado inasaka dawa ya kuondoka na
wadaiwa sugu wa mamlaka hiyo.
Amesema hadi sasa wanazidai taasisi
za serikali ikiwamo ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,Chuo cha
taaluma ya polisi(MPA) na Magereza mkoa zaidi ya shilingi Bilioni 1.7.
Amesema pamoja na kuzikatia huduma
ya maji taasisi hizo na baadaye kuzirejeshea huduma hiyo,hakuna dalili zozote
za kulikwa kwa malimbikizo hayo ya Ankara za maji kutokana na wakuu wa taasisi
hizo kudai hawana pesa.
“Tunaona suluhisho la yote haya ni
kuwafungia mita za maji ili kubaini kiwango cha matumizi yao na sasa tupo
katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato huo na tunaamini tukifanya hivyo
tutakuwa tumekata mzizi wa fitina”,alisema.
Mara kwa mara mamlaka hiyo imekuwa
ikichukua hatua za kusitisha huduma ya maji safi kwa taasisi hizo za serikali
kutokana na ukubwa wa malimbikizo ya madeni hayo lakini huishia kuendelea kutoa
huduma kutokana na unyeti wa taasisi hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni