Na Charles
Ndagulla,Moshi
WATU watatu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya
mwanafunzi Humphrey makundi(16) wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya
Scolastica iliyopo katika mji mdogo wa Himo,leo wamefikishwa mahakamani
wakikabiliwa na shitaka moja la mauaji.
Washitakiwa
hao ni pamoja na mmoja wa wakurugenzi wa shule hiyo,Edrwad Shayo,Mwalimu wa
shule hiyo Laban Nabiswa pamoja na mlinzi wa shule hiyo,Hamis Chacha.
Walisomewa
shitaka hilo na wakili wa serikali Cassim Nasri akisaidiwa na wakili wa Serikali Faygrace Sadallah mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya Julieth
Mawole .
Akisoma hati
ya mashitaka,wakili Nasri alidai kuwa,mnamo Novemba 6 mwaka huu huko maeneo ya Himo wilaya ya Moshi,washitakiwa kwa pamoja walimuua
kwa makusudi mtu mmoja aitwaye Humphrey Makundi.
Baada ya
kusomewa shitaka hilo,washitakiwa hao hawkautakiwa kujibu chochote kutokana na
mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji hadi
mahakama kuu.
Washitakiwa
walipelekwa mahabusu kwenye gereza kuu la mkoa,Karanga na kesi hiyo itatajwa
tena mahakamani hapo Decemba nane mwaka huu huku vilio vikitawala mara baada ya
washitakiwa hao kusomewa shitaka lao.
Mshitakiwa
wa pili na mmoja wa wamiliki wa shule hiyo,Edward Shayo alishindwa kujizuia na
kumwaga chozi muda mfupi baada ya kutoka mahakamani huku akiwapa wosia
ndugu zake akiwataka wamwombee kwani anaamini mungu yupo na atatenda muujiza.
Shayo
alifikishwa mahakamani hapo peke yake saa 5:39 akiwa ndani ya gari la polisi lenye
namba za usajili T367 CAF aina ya Toyota landCruser akitokea Hospital ya Rufaa
ya KCMC ambako amekuwa akipatiwa matibabu tangu kukamatwa kwake na alipanda
kizimbani pamoja na wenzake saa 7 :11 mchana .
DONDOO ZA TUKIO LILIVYOKUWA
1.Novemba 6
mwaka huu mwanafunzi huyo alidaiwa kutoweka shuleni hapo
2.Novemba 10
mwaka huu mwili wake uliokotwa ndani ya Mto Wona na kupelekwa chumba cha
kuhifadhia maiti katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa,Mawenzi
3.Novemba 12
mwili wa marehemu ulizikwa na Manispaa ya Moshi katika makaburi ya Karanga
baada ya kutojitokeza ndugu wa kuutambua
4.Novemba 17
mwaka huu mahakama ya hakimu mkazi mjini moshi ilitoa kibali cha mwili huo
kufukuliwa baada ya ndugu wa marehemu kubaini kuwa mwili uliozikwa katika
makaburi hayo ni wa mtoto wao.
MWILI WAFANYIWA UCHUNGUZI
Mwili wa
marehemu Humphrey ulifanyiwa uchunguzi na madaktari katika Hospital ya rufaa ya
KCMC na kushuhudiwa na Baba mzazi wa marehemu na katika uchunguzi
huo,ikibainika marehemu alikatwa na kitu chenye ncha kali
kiunoni,mgongoni,kwenye mapaja na mbavu mbili zilivunjika.
Baba mzazi huyo akawaeleza wanahabari kuwa kulingana na majibu ya uchunguzi huo ni ukweli ulio wazi kuwa,mwanaye aliuawa na kwamba kifo chake kinatia shaka na kuvitaka vyombo vya uchunguzi kuwasaka wahusika wa mauaji ya mtoto wake mpendwa.
Baba mzazi huyo akawaeleza wanahabari kuwa kulingana na majibu ya uchunguzi huo ni ukweli ulio wazi kuwa,mwanaye aliuawa na kwamba kifo chake kinatia shaka na kuvitaka vyombo vya uchunguzi kuwasaka wahusika wa mauaji ya mtoto wake mpendwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni