By
Daniel Mjema,Mwananchi
DODOMA.Waziri
wa Maliasili na Utalii,Dk.Hamis Kigwangala amemlipua waziri wa zamani wa
wizara hiyo,Lazaro Nyalandu akimtuhumu kwa matumizi mabaya ya madaraka.
Akichangia
mpango wa wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018,Dk Kigwangala ameiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu.
Kigwangala
amesema Nyalandu aliikosesha serikali mapato ya shilingi Bilioni 32 kwa miaka
miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hotel za
kitalii.
Mbali
na tuhuma hizo,pia alimtuhumu kutumia helkopita ya mwekezaji mmoja raia wa
kigeni kipindi cha kampeni zake za
kugombea urais 2015,wakati kampuni ya raia huyo ikituhumiwa kwa ujangili.
Hata
hivyo wakati Kigwangala akitoa tuhuma hizo,tayari Nyalandu alishasema kuwa
tuhuma ambazo zimeanza kuibuliwa mitandaoni dhidi yake si za kweli bali
zinalenga tu kumchafua.
Akizungumza
na mwananchi hivi karibuni ,alishangaa iweje ziibuliwe sasa zaidi ya miaka
miwili tangu aachie uwaziri.
LEMBELI
ALIVYOMSHUKIA NYALANDU
Machi
8 mwaka 2015,aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya
Ardhi,Maliasili na mazingira,James Lembeli,alimshutumu vikali Nyalandu
akimtuhumu kugeuza wizara hiyo
kama ofisi yake binafsi.
Lembeli
alitoa shutuma hizo mkoani Morogoro muda mfupi kabla ya kamati hiyo kupokea
taarifa ya uhifadhi kutoka kwa uongozi wa hifahdi ya Taifa ya Mikumi.
Shutuma
hizo zilikuja baada ya aliyekuwa mbunge wa Viti maalumu kwa wakati huo Ester Bulaya
kupitia kundi la vijana kutoka mkoa wa Mara(sasa yuko Chadema) kutaka wabunge
wapewe nakala ya tangazo la serikali(GN) linalohusiana na tozo mpya kwenye
hoteli za kitalii zilizopo kwenye hifadhi za Taifa.
Nyalandu
alisaini tangazo hilo la serikali februari 27 mwaka 2015 baada ya kuwapo na
msuguano wa muda mrefu na wabunge ambao kwa muda mrefu walikuwa wakimshutumu kwa kushindwa kutekeleza amri
ya mahakama kuu kuhusiana na tozo hizo mpya.
Lembeli
alihoji kitendo cha Nyalandu kuendesha
vikao na wamiliki wa hoteli hizo licha ya mahakama kuamulu wamiliki wa hoteli
hizo kulipa tozo mpya kama zilivyopendekezwa na shirika la hifadhi za
taifa,Tanapa.
“Uliona
wapi maamuzi ya mahakama yanajadiliwa nje ya mahakama,kulikuwa na nini
hapo?,tunafahamu kilichokuwa kinaendelea,sisi ndiyo tunaisimamia wizara hii
siyo watu wa nje?,alihoji .
Lembeli
alisema kuwa wizara ya maliasili na
utalii imekuwa kama ofisi ya mtu binafsi na kuongeza kuwa umefika wakati
wabunge wasema hapana, imetosha na hakuna cha utatu mtakatifu katika hilo.
Kwa
upande wake Bulaya alitaka wabunge wapewe nakala hiyo ya tangazo la serikali
ili waone kama kilichosainiwa kinaendana na yaliyomo kwenye uamuzi wa mahakama
na kuonya kuwa bunge lingewaka moto kama Nyalandu alisaini tofauti na uamuzi wa
mahakama.
Kutoka
na msuguano huo,wajumbe wote wa kamati hiyo walipitisha azimio la kumtaka
Nyalandu kuwasilisha nakala hiyo kwa kamati hiyo katika majumuisho ya ziara yao
ambayo yalifanyika Jijini mwanza.
Mgororo
huo wa tozo mpya katika hoteli za kitalii zilizopo kwenye hifadhi za tiafa
ulikolezwa na hatua ya Nyalandu kugoma kutekeleza maamuzi ya mahakama kuu
akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu uliofanywa na wataalamu wa Shirika la
Hifadhi za taifa,Tanapa.
Katika
kujitetea huko,Nyalandu alidai kuwa baadhi ya Hotel hazikujumuishwa katika
mchakato wa ulipaji wa tozo hizo mpya na kwamba tozo hizo zingeweza kukusanywa
kwa hotel 27 tofauti na hotel 56 zilizopo ndani ya hifadhi hizo.
Mkurugenzi
mkuu wa TANAPA,Allan Kijazi alisema kuwa hatua ya shirika lake kutaka
wenye hoteli hizo kulipa tozo mpya ni kutokana na wenye hotel hizo kupandisha
gharama za malazi kwa wageni kwa kila kitanda.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi huyo,awali Tanapa ilikuwa ikitoza kati ya dola 4 hadi 8
kwa kitanda kutokana na wageni kutozwa dola kati ya 100 hadi 150 kwa kitanda na
wenye hoteli.
Alisema
kuwa wenye hoteli hizo walipandisha tozo kwa wageni na kutoza kati ya dola 350
hadi dola 1,000 kwa kitanda hivyo shirika hilo kuamua kupendekeza tozo
mpya za kati vya dola 30 na 70 ambazo wenye hotel hizo walizigomea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni