Baba mzazi wa marehemu Humphrey makundi ,Jackson Makundi(katikati)akijadili jambo na ndugu zake wakati zoezi la kuufukua mwili wa mwanaye likiendelea katika makaburi ya Karanga mjini Moshi hivi karibuni.
Na Charles Ndagulla,Moshi
MAZISHI ya mwanafunzi,Humphrey Makundi(16) wa shule
ya Sekondari ya Scolastica iliyopo katika mji mdogo wa Himo anayedaiwa kupigwa
na kitu chenye ncha kali,yamekwama kufanyika jumamosi hii.
Kukwama kwa
mazishi hayo kunatokana na kuchelewa kutoka kwa majibu ya vipimo vya
vinasaba(DNA)vilivyopelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali na sasa mazishi hayo
yatafanyika wiki ijayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari wiki hii mjini hapa,Baba mzazi wa marehmu,Jackson
Makundi alisema kuwa wanatarajia kupata majibu ya vipimo hivyo wiki ijayo na
baada ya kutoka kwa majibu hayo,tararibu za mazishi zitafanyika mapema
iwezekanavyo.
“Tunaomba
uchunguzi ufanyike haraka na majibu ya vipimo yatoke haraka ili niweze kumzika
kwa heshima mtoto wangu,kwakweli ameteseka sana”,alisema makundi katika mkutano
wake na vyombo vya habari.
Mwanafunzi
huyo aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika shule hiyo,anadaiwa kutoweka
shuleni hapo asubuhi ya Novemba saba na mwili wake kupatikana Novemba 10 ukiwa
ndnai ya mto Wona mita 300 kutoka shule hapo.
Mwili huo
unadaiwa kukutwa na majeraha kichwani hali inayodhihirika kuwa kabla ya kifo
chake marehemu aliteswa kwa kupigwa na kitu kizito kilichopasua fuvu lake.
Baba mzazi
wa marehemu alisema katika mkutano wake na wanahabari kuwa,kwa mujibu wa
taarifa aliyopewa na daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili huo,mwanye alipigwa
na kitu chenye ncha kali na kupasua fuvu na kukana taarifa zinazoenezwa kuwa alikufa
kwa maji.
Hadi sasa
jeshi la polisi linawashilia zaidi ya watu 11 kwa mahojiano akiwamo mmiliki wa
shule hiyo,Edward Shayo wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo ambayo yameutikisa
mji wa Himo na mkoa mzima wa Kilimanjaro.
Mauji hayo
pia yamelaaniwa na baadhi ya wazazi wenye watoto wanaosoma katika shule mbali
mbali za bweni huku wakitilia shaka usalama wa watoto wao na kuzitaka mamlaka
husika kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na kuwafikisha mahakamani
watakaobainika kutenda unyama huo.
Wengine
wanaoshikiwa yumo mlinzi wa shule hiyo anayedaiwa kumpiga na kitu kizito marehemu,wamo
daktari katika hopsital ya mkoa,mawenzi wanaodaiwa kufanya udanganyifu kuhusu
umri wa marehemu na kutoa kibali cha kuuzika mwili huo chap chap.
Kwani hii blog bado inafanya kazi ndagula, naomba tutumie habari bwana, Stambuli- 0655339616
JibuFuta