Jumapili, 4 Mei 2014

WANAHABARI IRINGA WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA


Katibu  wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin wa pili  kulia  akiongoza  wanahabari na wananchi wa kata ya Ilala kwenda kufanya usafi wa mazingira   leo  wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.

Wanahabari  mkoa wa Iringa  wakiadhimisha siku ya uhuru wa  vyombo vya habari kwa kufanya usafi.
Hapa  wakiendelea  kuzoa takataka

Wananchi  waliounga  mkono jitihada hizo

Mitaa mbali mbali ya Ilala usafi  ukifanywa na  wananchi kuunga mkono siku ya uhuru wa vyombo vya habari  jana
Na Diana Bisangao ,Iringa

WANAHABARI  mkoa  wa  Iringa  waungana na  wakazi wa kata  ya Ilala katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa waadhimisha  siku ya uhuru wa  vyombo  vya habari duniani kwa    kufanya usafiri wa mazingira  katika  kata  hiyo ya Ilala inayoongozwa na naibu  meya wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Grevas Ndaki.

Mbali ya  wanahabari  hao  kushiriki  kuzoa taka katika eneo hilo la Ilala  pia  wamefikisha neema kwa wananchi hao wa Ilala baada ya  kuwaombea chombo maalum cha  kuhifadhia taka (DAMPO) ambacho  walikuwa hawana na kulazimika kutupa katakata katika kiwanja cha mkazi mmoja wa eneo  hilo.

Wakizungumzia utaratibu  huo  wa wanahabari Iringa kujitolea  kufanya  usafi wa mazingira  baadhi ya  wananchi  wa kata  hiyo ya Ilala  walisema kuwa kilichofanywa na wanahabari  hao ni mfano wa kuigwa na  kuwa kwani  ni kwa  mara ya kwanza katika  kata  hiyo  wanashuhudia wanahabari hao  wakionyesha  mfano wa kushika vifaa vya usafi na kuzoa taka badala ya  kuandika pekee.

Alisema Amina Sanga  kuwa  baada ya  kusikia katika  vyombo  vya habari  jana  kuwa  wanahabari hao  wangefika  kufanya  usafi katika  eneo  lao  wengi  wao  walikuwa na  hamu ya  kushuhudia kama ni kweli  wanahabari  hao  watafika  kufanya usafi  ila  baada ya  kuwaona  wao kama  wananchi  walifarijika  zaidi .

Huku kwa  upande  wake  Husein Ally  alisema kuwa changamoto  kubwa  ya  usafi katika  eneo hilo ni kukosekana kwa chombo  cha kuhifadhia  taka na  hivyo kuwafanya  wananchi  kutupa takataka  eneo la uwanja  wa  mtu jambo ambalo kiafya ni hatari  zaidi kwani  wapo  baadhi ya  watoto  wamekuwa  wakishinda katika takataka hizo kuokota  uchafu  huo na kuchezea.

Hivyo  waliomba  wanahabari  hao  kuwasaidia  kuwaombea chombo  cha kuhifadhia  takataka  ili  kiweke eneo hilo na kila kinapojaa  basi gari la kubeba  uchafu la Manispaa kufika  na kuziondoa mapema.

Katibu  mtendaji  wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa wa Iringa (IPC)  Bw Francis  Godwin alisema  kuwa kitaifa  maadhimisho  hayo yamefanyika mkoani Arusha ambapo  mwenyekiti  wake Frank  Leonard amekwenda  kuwawakilisha  wanahabari  wa  mkoa  wa Iringa ambapo kauli mbinu kwa  mwaka  huu kitaifa ni  Uhuru wa Habari kwa maendeleo na  utawala  bora .

Godwin  alisema  kuwa  mbali ya kauli mbinu  hiyo ya kitaifa  mkoa  wa Iringa umeongeza kauli mbinu ya  pili  kwa ajili ya mkoa   huo mbali ya ile ya Taifa  pia wamejiongezea ile ya uhuru wa vyombo vya habari  na  usafi wa mazingira  ni jukumu letu sote .

Hivyo  alisema kuwa kutokana na heshima kubwa ya mkoa wa Iringa  iliyopata  kupitia Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa kwa kuwa ya  pili kiusafi  kitaifa  wao wameamua kuunga mkono jitihada hizo kwa kuhamasisha jamii  kufanya  usafi katika mji  huo .

Pia  kujitolea misaada mbali mbali kwa  kituo cha Yatima  cha DBL Mkimbizi  na kuwa  suala  hilo la usafi katika kata ya Ilala  limefanyika kama  sehemu ya  kuihamasisha  jamii  kuendelea  kufanya usafi katika maeneo yao .

Aidha  aliomba uongozi wa Manispaa kuunga mkono  jitihada hizo kwa  kuweka Dampo eneo hilo la Ilala ili kuwawezesha  wananchi hao kuwa na sehemu ya kuhifadhi takataka.

Afisa  msimamizi  wa  wahudumu wa usafi  katika Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Aron Mafumiko  mbali ya kuwapongeza wanahabari  hao kufika kufanya usafi  pia  alikubali kuweka dampo la kudumu eneo hilo la Ilala  kama  sehemu ya kuunga mkono jitihada za wanahabari hao mkoa wa Iringa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni