Na Charles
Ndagulla,Moshi.
MTUMISHI
mmoja wa benki ya kibiashara ya Mkombozi tawi la Moshi(jina
tunalihifadhi),anatuhumiwa kuiba zaidi ya shilingi Milioni 57 kutoka kwenye
akaunti za wateja wa benki hiyo.
Habari za
uhakika ambazo mtandao huu umezipata zimedai kuwa,mtumishi huyo aliiba fedha
hizo kati ya Oktoba na Desemba mwaka jana lakini polisi wameshikwa kigugumizi
kuanika majina ya wateja waliolizwa fedha zao.
Taarifa
kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali mjini Moshi,zinapasha kuwa,polisi
wamekataa kuweka wazi majina ya wateja hao,akaunti zao na kiasi cha fedha
kilichoibwa na mtumishi huyo.
Inadaiwa
kuwa,kugoma kwa polisi kuweka majina ya wateja hao,kumeikwamisha ofisis hiyo ya
mwanasheria mkuu wa serikali kuandaa hati ya mashitaka ili mtumishi huyo aweze
kufikishwa makahamani.
Hata hivyo taarifa zinapasha kuwa,mtumishi huyo hakuweza kunufaika na mamilioni hayo ya wateja baada ya kuingizwa 'mjini' na matapeli waliomhadaa kuwa fedha hizo zitaongezeka mara dufu.
Kwa lugha nyepesi mtumishi huyo aliponzwa na uroho wa kupata utajiri wa chap chap bila kuutolea jasho na sasa yupo kikaangoni kwani anakabiliwa na tishio la kufukuzwa kazi wakati wowote.
Kwa taarifa zaidi juu ya sakata hilo enedelea kutembelea mtandao huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni