Jumatano, 3 Januari 2018

MTUMISHI P P F ALIYENASWA NA DAWA ZA KULEVYA NGOMA NZITO

  Na Charles Ndagulla,Moshi
 
MTUMISHI wa mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa (PPF),Anitha Osward(32),anayetuhumiwa kujihusisha na usafrishaji wa dawa za kulevya,bado anasota katika mahabusu ya jeshi la polisi ikiwa ni siku ya 16 leo tangu alipokamatwa  bila kufikishwa mahakamani.
 

Mtumishi huyo,alikamatwa desemba 19 mwaka jana akiwa na shehena ya madawa ya kulevya aina ya mirungi aliyokuwa akiisafrisha kwa kutumia gari lake dogo aya ya Toyota Sienta lenye namba za usjaili T674DLB.

 Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,Hamis Issah,mtuhumiwa huyo  bado anashikiliwa na jeshi la polisi mpaka sasa ., 
 
Kamanda Issah amesema jalada la uchunguzi wa tuhuma hizo lipo kwa mwanasheria mkuu wa serikali kwa ajli ya mapitio kabla ya kuandaliwa hati ya mashitaka.
 
kwa mujibu wa Kamanda Issah,polisi itaendelea kumshikilia mtuhumiwa huyo hadi hapo jalada lake litakapokuwa tayari kutokana na kesi zinazohusiana na usafrishaji wa dawa za kulevya kutokuwa na dhamana.
 
  Anitha Osward,mtuhumiwa wa dawa za kulevya
 
 
 
“Askari wakiwa doria walimkamata Anitha Oswald, ambaye ni mkazi wa Karanga, Manispaa ya Moshi, akiwa anasafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 216 na gramu 370”, alisema kamanda Issa. 
Kamanda Issa alisema Anitha Oswald alikamatwa eneo la Majengo kwa Mtei Disemba 19, mwaka jana, akiwa anatokea Njia Panda ya Himo kuchukua mzigo huo. 
Aidha kamanda Issa alisema kwamba usafirishaji wa dawa za kulevya bado ni changamoto kubwa ambapo alielezea kusikitishwa na tabia ya baadhi ya watumishi wa Umma kujihusisha na usafirishaji huo.
“Jeshi la polisi mkoani hapa liko makini, operesheni inaendelea na hatutamvumilia mtu yeyote ambaye atabainika kujihusisha na biashara hii”, alisema.
Hata hivyo kamanda aliongeza kusema kwamba jeshi hilo la polisi mkoani kilimanjaro, bado linaendelea kumtafuta dereva wa gari hilo, ambaye alikimbia baada ya kulitelekeza gari alilokuwa akiliendesha baada ya kugonga mti katika jitihada za kuwakimbia polisi.
 
Mtuhumiwa wa dawa za kulevya,Anitha Osward akiwa amesimama mbele ya gari lake aina ya Toyota Sienta lenye namba za usajili T674 DLB,huku shehena ya dawa za kulevya aina ya Mirungi ikiwa ndani ya gari lake.
Pichani ni mifuko iliyosheheni madawa ya kulevya aina ya mirungi ambayo ilikamatwa na polisi desemba 19 mwaka jana,tayari polisi wanamshikilia mtumishi wa mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma(PPF),Anitha Osward akituhumiwa kusafrisha shehena hiyo kwa kutumia gari lake binafsi aina ya Toyota Sienta lenye namba za usajili T674 DLB.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni