Na Charles Ndagulla,Moshi.
MCHUNGAJI Zakaria Donald Yona wa
Kanisa la Yesu Anaweza Centre ameingia matatani akituhumiwa kuishi nchini
isvvyo halali baada ya kudaiwa kuwa ni raia wa Kenya.
Uchunguzi wa mtandao huu umebaini kuwa,mchungaji huyo ni raia wa Kenya
kwa kuzaliwa lakini mwenyewe amekana tuhuma hizo na kudai ni mtanzania
kwa kuzaliwa.
Kwa mujibu wa nyaraka ambazo mtandao
wa NdagullaBlog umeziona zinaonyesha kuwa,mchungaji huyo anayeendesha kanisa
lake eneo la Mji Mpya Manispaa ya Moshi,alizaliwa mwaka 1964 eneo la
Siaya mkoa wa Nyanza nchini Kenya.
Kulingana na nyaraka hizo,baada ya
kuzaliwa alipewa cheti chenye namba ya ingizo 4300247/85 akitambuliwa kwa
majina ya Donald Oloo Waswani huku pia akiwa na kadi ya utaifa wa Kenya yenye
namba 237104963 iliyotolewa Oktoba 10 mwaka 2013.
Pia mke wa mchungaji huyo anayetumia
majina ya Redempter William Francis kwa hapa nchini,uchunguzi umebaini kuwa
alizaliwa mwaka 1970 huko Machakos nchini Kenya huku akiwa na kadi ya uraia wa
nchi hiyo yenye namba 223854431 iliyotolewa mwaka 2007.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa,mchungaji huyo amesajiliwa kama
mlipa kodi na mamlaka ya mapato nchini Kenya(KRA) na kupewa namba ya
utamburisho wa mlipa kodi(Personal Identification Number) Na A.010329470.
Mchungaji huyo na mkewe Redempter
William Francis,wanadaiwa kufunga ndoa yao Oktoba 13 mwaka 1991 katika Kanisa
la Dandora Gaspel Tabernacle na kupewa cheti chenye namba 465369.
Hata hivyo mchungaji huyo
amezungumza na NdagullaBlog na kutupilia
mbali tuhuma hizo lakini akishindwa kuweka wazi ni wapi alipozaliwa
akidai wakati ukifika ataweka wazi kila kitu.
“Suala la mimi nimezaliwa wapi
tutakuja kuliweka sawa lakini kwa ufupi mimi ni mtanzania kwa kuzaliwa na hayo
mengine yote yatajulikana huko mbele ya safari”,alisema .
Wakati mchungaji huyo akikwepa
kuweka wazi alikozaliwa,NdagullaBlog imefanikiwa kuona nyaraka mbalimbali
baadhi zikidaiwa ni za kughushi zikionyesha mchuangaji huyo alizaliwa Nyamagana
mkoani mwanza mwaka 1964.
Kwa mujibu wa cheti cha kuzaliwa
kilichosajiliwa Machi 15 mwaka 2010,kinaonyesha mchungaji huyo alizawali eneo
hilo na kusajiliwa kwa jina la Zacharia Donald Yona Munuo.
Pia mkewe ambaye kwenye cheti cha
kuzaliwa nchini Kenya anatumia majina ya Redempter Ndinda Nthenge,kwenye cheti
cha kuzaliwa hapa nchini anatambulika kwa majina ya Dedempter William Francis
Munuo akidai alizaliwa Nyamagana mkoani Mwanza mwaka 1969.
Wawili hao pia wanadaiwa kufunga
ndoa ya kiserikali mkoani Kilimanjaro Juni 13 mwaka 2007 na kupewa cheti
B/N na.0748488 hali ambayo inazidisha utata zaidi juu ya uraia wa wawili hao.
Mchungaji huyo amekiri kuwahi
kukamatwa yeye na familia yake yote na maofisa wa jeshi la uhamiaji mkoani
Kilimanjaro na kufikishwa makahamani akidaiwa kuishi nchini isivyo halali.
“Tulikamatwa juni 20 mwaka jana na
wakatushikilia kwa siku mbili na baadaye wakatupeleka mahakamani,madai yao ni
kwamba mimi na familia yangu si raia wa Tanzania bali ni raia wa Kenya”,amedai.
Amedai kuwa,uhamiaji walidai kuwa
wangepeleka mashahidi 15 na vielelezo zaidi ya 20 kudhibitisha kuwa mchungaji
huyo si raia wa Tanzania lakini hawakufanya hivyo.
Hata hivyo mchungaji huyo amesema
kuwa,uhamiaji waliondoa shauri hilo mahakamani desemba 6 mwaka jana baada
ya kudai upande wa jamhuri hauna nia tena ya kuendelea kuwashitaki.
Mchungaji huyo amedai kuwa,wakati
wakiamini suala hilo limeisha na wako huru kuendelea na maisha yao,walijikuta
wakikamatwa tena nje ya mahakama na kupelekwa ofisi za uhamiaji .
Kwa mujibu wa mchungaji huyo,baada
ya kufikishwa katika ofisi hizo walilazimishwa kusaini nyaraka za kuondolewa
nchini na walipokataa kusaini nyaraka hizo waliondolewa nchini kwa nguvu na
kupelekwa mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Holili.
“Tulipofika holili maofisa wa
uhamiaji wa Kenya walikataa kutupokea baada ya uhamiaji Tanzania kukosa nyaraka
mhimu kuonyesha sisi hatutakiwi Tanzania zikiwamo nyaraka za mahakama”,amesema.
Mchungaji huyo amesema kuwa baada ya zoezi hilo kugonga mwamba,maofisa hao
wa uhamiaji waliamua kuwatelekeza mpakani na kuondoka kabla ya mchungaji huyo
na familia yake kuamua kurejea nyumbani kwa kutumia usafiri mbadala.
Msemaji wa uhamiaji mkoani
Kilimanjaro(DCI),Albert Rwelamila amedhibitisha kuwepo na uchunguzi unaofanywa
na ofisi yake juu ya uhalali wa uraia wa mchungaji huyo na familia yake
alipozungumza na NdagullaBlog hivi karibuni.
Hata hivyo,Rwelamila hakuwa tayari
kulizungumzia suala hilo kwa undani zaidi kwa kile alichodai lipo zuio la
mahakama kuu linalowataka kusitisha mchakato huo hadi hapo suala hilo
litakapotolewa uamuzi.
“Ni mhimu tukaheshimu zuio la
mahakama maana ni chombo cha kisheria nadhani baada ya kusikiliza pande zote na
kutoa uamuzi hapo tunaweza kuwa na cha kusema,kwa sasa tuliache
kwanza”,alisema.
NdagullaBlog imeambiwa kuwa,zuio
hilo limewekwa baada ya mchungaji huyo kukimbilia mahakama kuu desemba 15 mwaka
jana kupitia kwa wakili wake Caessar Shayo.
Kwa upande wake wakili Shayo amesema
kuwa hati ya zuio ilitolewa desemba 18
mwaka jana na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Moshi,Aishiel Sumari.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni