Na Charles
Ndagulla,Moshi
MFANYABIASHARA na mzaliwa wa Kijiji cha Uchau Kaskazini
wilaya ya Moshi Vijijini,Emmanuel Mallya,ameikabidhi serikali zahanati ikiwa na
vifaa vya kisasa vikiwamo vitanda vya wagonjwa vinavyotumia nishati ya umeme.
Zahanati
hiyo inayojukana kwa jina la EB zahanati,imejengwa na mfanyabiashara huyo kwa
kutumia nguvu zake mwenyewe bila kuhusisha msaada kutoka Halmashauri ya wilaya
ya Moshi wala serikali kuu.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kuikabidhi zahanati
hiyo kwa serikali,mfanyabiashara huyo alisema wazo la kujenga zahanati
hiyo lilitokana na kuwepo na changamoto za umbali wa huduma za afya kwa wananchi
wa eneo hilo.
Alisema changamoto
hiyo ilipelekea kuwepo na vifo vya watu wengi vilivyochangiwa na umbali wa upatikanaji
wa vituo vya afya na kwamba changamoto hizo ndizo zilizomsukama kuona haja ya
kujenga zahanati hiyo.
Alitoa wito
kwa mamlaka husika kuitunza zahanati hiyo pamoja na vifaa vitakavyotumika
katika kuwahudumia wagonjwa huku akitoa wito kwa watu wengine wenye uwezo
kujitolea katika kuwahudumia wananchi wasio nacho.
“Utajiri
unatokana na moyo wa mtu alionao,unaweza ukawa na utajiri na usiwe na moyo wa
kuwasaidia wengine,kila mtu amepewa karama na mwenyezi mungu,mhinu hapa ni
namna ya kuzitambua hizo karama”,alisema.
Kabla ya
ujenzi huo ulioanza julai mwaka 2013,familia iliyokuwa ikishi mahali
ilipojengwa shule hiyo iliridhia ombo la mfanyabaishara huyo la kuachia eneo
hilo na kupelekwa kwenye eneo jingine kwa ushirikiano wa Chama cha Msingi cha
Ushirika cha Kimasio.
Aliwapongeza
familia hiyo kwa kukubali ombi lake la kuliachia eneo hilo na kuongezak
uwa,bila familia hiyo kiridhia kuondoka katika eneo hilo ndoto zake za kujenga
zahanati katika eneo hilo zingeshia ukingoni.
Mbunge wa
Jimbo la Moshi Vijijini,Anthony Komu alihimiza usimamizi wa karibu wa zahanati
hiyo kwa wale watakakuwa wasimamizi baada ya aliyeijenga kuikabidhi kwa
serikali.
"Mheshimiwa
mkuu wa wilaya,uzoefu unaonyesha kuwa,miradi mingi inayojengwa na wafadhili
imekuwa ikiharibikak utokana na kutokuwepo na usimamizi wa karibu,ni rai yangu
kuwa tuitunze zahanati hii isijekuwa mazalia ya popo kama ambavyo tumekuwa
tukishuhudia kwa baadhi ya zahanati na vituo vya afya”,alisema.
Alisema
mfanyabiashara huyo ametenda wema wa hali ya juu kwa wananchi wa wilaya ya
Moshi Vijijini na Vunjo kwa ujumla na
kwamba wema huo kamwe hautafutika ndnai ya mioyo ya wananchi hao.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila(kulia)akitia saini makabidhiano ya EBZahanati iliyojengwa kwa msaada wa mfanyabiashara Emmanuel Mallya,kutoka kushoto na mke wa Emmanuel Mallya pamoja na Mallya mwenyewe wakitia saini makabidhiano hayo hivi karibuni.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Michael Kilawila,alitoa wito
kwa wananchi wa wilaya hiyo kuchangishana kwa kile kidogo walichonacho ili
wanunue gari la wagonjwa ambalo litahudumia zahanati hiyo kwa muda wa saa 24.
Alisema uwepo
wa gari la wagonjwa katika zahanati hiyo utarahisisha kuwapeleka wagonjwa
katika Hospitla kubwa ikiwamo ya Kibosho,Mawenzi na KCMC kwa wale ambao
watahitaqji kupewa rufaa.
Alisema
maendeleo yanahitaji umoja na mshikamano
nak uonya kuwa maendeleo hayana itikadi yoyote ya kisiasa kwani zahanati hiyo
itahudumia wananchi wote bila kujali huyu ni wa chama gani.
Utiaji saini makabidhiano ya EB Zahabati ukiendelea,zahanati hiyo imejengwa na mfanyabiashara Emmanuel Mallya ambaye pia ni mzaliwa wa Kibosho wilaya ya Moshi.
Akizungumza
katika hafla hiyo,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba,alipongeza moyo
ulioonyeshwa na mfanyabiashara huyo wa kusaidia watu wenye mahitaji .
Mkuu huyo wa
wilaya alitoa wito kwa serikali ya kijiji hicho kuanza mazungumzo na wananchi
wanaoishi karibu na zahanati hiyo ya kuachia maeneo yao ili zahanati hiyo
ipanuliwe na kufika hadhi ya kituo cha Afya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila(kulia)wabadirishana hati na Mfanyabiahara Emmanuel Mallya muda mfupi baada ya utilianaji sani makabidhiano ya EB Zahanati iliyojengwa na mfanyabiashara huyo katika kijiji cha Uchau Kaskazini wilaya ya Moshi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni