Na
Kija Elias, Hai.
Baraza
la Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, limepitisha sheria
ndogo ndogo zikiwemo sheria za vibali vya ujenzi vinayomtaka kila mwananchi
ambaye anataka kujenga lazima awe na kibali cha ujenzi huo.
Sheria
hiyo imepitishwa jana, kufuatia agizo lililotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ambalo alilitoa hivi karibuni la
kuwataka viongozi wa Halmashauri za wilaya,miji Majiji nchini, kuharakisha
utoaji wa vibali vya ujenzi na kuachana na urasimu ambao ulikuwa ukisababisha
kuwepo kwa ujenzi holela.
Akisoma
sheria hizo kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Afisa Ardhi wa wilaya
hiyo Jacob Muhumba, alisema kuwa mtu yeyote atakaye jenga bila kuwa na kibali
cha ujenzi sheria hiyo imeweka adhabu kali ikiwa ni pamoja na kusitisha ujenzi
wake na kufikishwa katika vyombo vya dola.
“Sheria
hii inamtaka kila mtu anayetaka kujenga ni lazima awe na kibali cha ujenzi,
hatutamruhusu mtu kujenga bila kuwa na kibali, na kila mtu atakayekuwa anaomba
kibali cha ujenzi atalazimika kulipia gharama kwa ajili ya kupata kibali
hicho,”alisema Muhumba.
“Tulikuwa
hatuna sheria ya vibali vya ujenzi tangu zamani, lakini pia tulikuwa hatutozi
gharama yeyote ile, hivyo mwananchi alikuwa akijijengea tu bila kufuata
utaratibu hali ambayo imechangia kuwepo kwa makazi holela,”alisema.
Aidha
alifafanua kuwa gharama hizo za kupata kibali cha ujenzi kitategemea na kile
mtu anachotaka kujenga , ikiwemo ujenzi wa nyumba za makazi, maghala, viwanja
vya ndege na majengo ya biashara .
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Helgha Mchomvu alisema
kuwa baraza hilo limelazimika kuipitisha sheria hiyo ili kuepusha ujenzi
holela ambao umekuwa ukifanyika na hivyo kuufanya mji wa Bomang’omba kutokuwa
katika mpangilio mzuri.
Katika
hatua nyingine halmashauri hiyo ya wilaya ya Hai,imeshindwa kufikia lengo la
kukusanya mapato ya shilingi Bilioni 2.5 kutokana na baadhi ya vyanzo vya
mapato vya halmashauri hiyo kuchukuliwa na serikali Kuu.
“Ukusanyaji
wa mapato umeshuka kutoka bilioni 2.5 hadi kufikia bilioni 2.1 hii imechangiwa
na serikali kuu kuchukua vyanzo vyetu ambavyo tulikuwa tukikusanya, hivyo
kupitishwa kwa sheria ya kuwa na kibali cha ujenzi itasaidia kuongeza ukusanyaji
wa mapato,”alisema mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Wakizungumzia
hatua ya kuwepo na sheria ya vibali katika ujenzi wa nyumba baadhi ya wakazi wa
mji wa Boma ng’ombe, kuhusu wamesema kuwa itasaidia sana kwani kumekuwepo
na ujenzi holela ambao unachangia kuharibu mandhari ya mji huo.
Gidion
Lucas na Issaya Fabiani, walisema kumekuwepo na ucheleweshaji mkubwa wa kupata
vibali vya ujenzi unaosababishwa na wahusika wenyewe na hivyo kuchangia
wananchi kujenga kiholela bila kufuata utaratibu, kutokana na kuchoka
kusubiri kwa muda mrefu ili waweze kupata vibali vya ujenzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni