JESHI la
polisi mkoani Kilimanjaro,linamshikilia mtumishi mmoja wa shirika moja la Umma
mjini Moshi akituhumiwa kujihusisha na usafrishaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi.
Kamanda wa
polisi mkoani Kilimanjaro,Hamisi issah,amedhibitisha kukamatwa na kushikiliwa
kwa mtumishi huyo ambaye kwa sasa tunahifadhi jina lake baada ya kukamatwa na
shehena kubwa ya mirungi aliyokuwa akiisafrisha kwa kutumia gari lake dogo.
Mtumishi huyo
alikamatwa desemba 19 mwaka huu nje kidogo ya mji wa Moshi baada ya gari lake kuparamia
mti na kupata ajali akiwa katika jitihada za kuwakimbia polisi.
Kwa mujibu
wa Kamanda Issah,dereva wa gari hilo alitimua mbio na kumwacha mtumishi huyo wa
shirika la umma akitiwa mbaroni.
Taarifa
zaidi pamoja na picha za mtuhumiwa huyo zitafuata hivi punde
Kwa taarifa
juu ya mkasa huyo pamoja na majina kamili ya mtumishi huyo na taasisi
anayofanyia kazi endelea kutembelea mtandao huu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni