Maofisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ)wakiwa wamebeba moja ya jeneza lenye mwili wa askari wa jeshi hilo aliyekuwa miongozi mwa askri 14 waliouawa nchini Mamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) alhamis ya desemba 7 mwaka huu mara baada ya kuwasili nchini jana jumatatu desemba 11
Maofisa wa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ)wakiwa wamejipanga mstari tayari kuilaki miili ya askari 14 wa jeshi hilo waliouawa nchini DRC alhamis desemba 7 mwaka huu ilipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JKN Jijini Dar es salaam jana desemba 11
Ndege ya shirika la Umoja wa Mataifa(UN)iliyobeba miili ya askari 14 wa jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ)waliouawa nchini Kongo ikiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam jana desemba 11
Miili ya askari 14 wa jeshi la wananchi Tanzania ikiingizwa kwenye gari la jeshi hilo muda mfupi baada ya kuwasili kutoka nchini DRC,askari hao wanadaiwa kuuawa na waasi wa ADF alhamis desemba 7 mwaka huu wakiwa katika kikosi cha kulinda Amani cha Umoja wa mataifa
Umoja wa mataifa walaani shambulio dhidi ya walinda amani hao.
Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania
waliouawa wakati wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda
Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasili jijini Dar es Salaam,
Tanzania jumatatu desemba 11.
Miili hiyo ilisafirishwa kwa Ndege
za Umoja wa Mataifa kutoka nchini DR Congo na kupokelewa na maofisa wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi.
Waliuawa wakati wa shambulio
lililotekelezwa Alhamisi ya desemba 7 mwaka huu kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni
katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Wanajeshi wengine zaidi ya 50
walijeruhiwa.
Umoja wa Mataifa ulisema wanajeshi 5
wa jeshi la DR Congo (FARDC) waliuawa pia kwenye shambulio hilo
Waasi wa ADF ndio wanaotuhumiwa
kutekeleza shambulio hilo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Antonio Guterres alishutumu vikali shambulio hilo na kusema ni sawa na uhalifu
wa kivita.
Wanajeshi zaidi walitumwa eneo hilo na kamanda wa kikosi cha kulinda amani anaelekeza shughuli ya kuwaondoa majeruhi.
Bw Guterres alisema shambulio hilo ndilo mbaya zaidi kuwahi kutekelezwa dhidi ya walinda amani wa UN katika historia yake miaka ya karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni