Mmiliki wa shule ya sekondari ya Scolastica iliyopo Himo Mkoani Kilimanjaro,Edward Shayo na washitakiwa wenzake,Hamis Chacha na Laban Nabiswa wakiongozwa na polisi kwenda kizimbani tayari kusomewa shitaka la mauaji ya kukusidia ya mwanafunzi wa shule hiyo,Humphrey Makundi,kesi hiyo itatajwa tena desemba 22 mwaka huu
AANGUA KILIO KIZIMBANI
Na Charles Ndagulla,Moshi
MMILIKI wa shule binafsi ya
sekondari ya Scolastica iliyopo katika Mji wa Himo mkoani Kilimanjaro,Edward
Shayo jana aliangua kilio mahakamani baada ya kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa
shule hiyo inayomkabili yeye na wenzake wawili kupigwa kalenda
Shayo ambaye ni mshitakiwa wa pili
katika kesi hiyo amekuwa haamini kilichotokea kwani tangu aliposomewa shitaka la mauaji ya kukusidia kwa
mara ya kwanza Novemba 27 mwaka huu,amekuwa katika hali ya majonzi huku akitoa
raia kwa ndugu zake kumwombea.
Mbali na Shayo,washitakiwa wengine katika
kesi hiyo ya mauaji ni Hamis Chacha ambaye ni mlinzi wa shule hiyo pamoja na
Makamu mkuu wa shule hiyo,Laban Nabiswa .
Wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa
kosa moja la mauaji ya kukusidia dhidi ya aliyekuwa mwanafunzi wa shule
hiyo,Marehemu Humphrey Makundi(16)
anayedaiwa kuuawa Novemba 6 mwaka huu na mwili wake kutupwa mto Wona jirani na
shule hiyo.
Walisomewa shitaka hilo na wakili wa
serikali Cassim Nasri akisaidiwa na wakili wa Serikali Faygrace Sadallah mbele
ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya Julieth Mawole .
Akisoma hati ya mashitaka,wakili
Nasri alidai kuwa,mnamo Novemba 6 mwaka huu huko maeneo ya Himo wilaya ya Moshi,washitakiwa kwa pamoja walimuua
kwa makusudi mtu mmoja aitwaye Humphrey Makundi.
Baada ya kusomewa shitaka
hilo,washitakiwa hao hawakautakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo
kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji hadi mahakama kuu.
Washitakiwa walipelekwa mahabusu
kwenye gereza kuu la mkoa,Karanga na kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo
Decemba 22 mwaka huu huku vilio vikitawala mara baada ya washitakiwa hao
kusomewa shitaka lao.
DONDOO
ZA TUKIO LILIVYOKUWA
1.Novemba 6 mwaka huu mwanafunzi
huyo alidaiwa kutoweka shuleni hapo
2.Novemba 10 mwaka huu mwili wake
uliokotwa ndani ya Mto Wona na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika
Hospital ya Rufaa ya Mkoa,Mawenzi
3.Novemba 12 mwili wa marehemu
ulizikwa na Manispaa ya Moshi katika makaburi ya Karanga baada ya kutojitokeza
ndugu wa kuutambua
4.Novemba 17 mwaka huu mahakama ya
hakimu mkazi mjini moshi ilitoa kibali cha mwili huo kufukuliwa baada ya ndugu
wa marehemu kubaini kuwa mwili uliozikwa katika makaburi hayo ni wa mtoto wao.
MWILI
WAFANYIWA UCHUNGUZI
Mwili wa marehemu Humphrey
ulifanyiwa uchunguzi na madaktari katika Hospital ya rufaa ya KCMC na
kushuhudiwa na Baba mzazi wa marehemu na katika uchunguzi huo,ikibainika
marehemu alikatwa na kitu chenye ncha kali kiunoni,mgongoni,kwenye mapaja na
mbavu mbili zilivunjika.
Baba mzazi huyo akawaeleza wanahabari kuwa kulingana na majibu ya uchunguzi huo ni ukweli ulio wazi kuwa,mwanaye aliuawa na kwamba kifo chake kinatia shaka na kuvitaka vyombo vya uchunguzi kuwasaka wahusika wa mauaji ya mtoto wake mpendwa.
Baba mzazi huyo akawaeleza wanahabari kuwa kulingana na majibu ya uchunguzi huo ni ukweli ulio wazi kuwa,mwanaye aliuawa na kwamba kifo chake kinatia shaka na kuvitaka vyombo vya uchunguzi kuwasaka wahusika wa mauaji ya mtoto wake mpendwa.
SHULE
WASUSIA MAZISHI
Katika hali ya kusikitisha na kushangaza,uongozi wa
shule hiyo,ulisusia mazishi ya mwanafunzi huyo yaliyofanyika DEesemba 2 mwaka
huu katika Kijiji cha Komakundi wilaya ya Moshi Vijijini.
Uongozi wa shule hiyo haukuweza
kutuma mwakilishi katika mazishi hayo ambayo yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro,Anna Mgh’wira huku ibaada ya mazishi ikiongozwa na msaidizi wa
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma ,Mchungaji Samwel Mshana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni