TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na rushwa(Takukuru) mkoani Kilimanjaro,imewafikisha
mahakamani waliokuwa vigogo wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakituhumiwa kwa
makosa mbali mbali ikiwamo ya matumizi mabaya ya madaraka.
Washitakiwa
hao ni aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Melkezedeck Humbe ambaye kwa
sasa ni mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya yaBariadi mkoani Simiyu,aliyekuwa
mweka hazina wa halmshauri hiyo,Thadeus Meela na Valtine Mollel.
Taarifa za hivi punde zilizotufikia kutoka
Hai,washitakiwa hao muda si mrefu watasomewa mashitaka yao katika mahakama ya
hakimu mkazi wilaya ya hai .
Kwa taarifa
zaidi juu ya mashitaka yanayowakabili
vigogo hao tutakuletea muda si mrefu
Endelea kutembelea
mtandao wetu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni