Na Charles Ndagulla,Moshi
MAMLAKA ya Chakula la Dawa(TFDA)Kanda ya kaskazini,imekifunga kiwanda cha kutengeneza pombe aina ya Banna inayotengenezwa na Kampuni ya Derrick Global Trading(D.G.T ) cha mjini moshi kutoka na kubainika kuwa na kasoro .
Kiwanda hicho kimefungwa chini ya
kifungu cha 181 sura ya 209 ya sheria ya chakula na dawa ya mwaka 2003 kutokana na tuhuma za kutumia nembo ya kiwanda kingine cha kutengeneza pombe kali kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari
kiwandani hapo,Mkaguzi wa chakula mwandamizi kutoka TFDA Kanda ya
kaskazini,William Mhina,alisema sababu nyingine za kufungwa kwa kiwanda hicho ni
mazingira yasiyoridhisha ya kiwanda hicho.
Alitaja sababu zingine ni
wafanyakazi kutokuwa na vyeti vya kuonyesha afya zao huku wafanyakazi hasa wa
kike kutokuvaa kofia kichwani.
Alisema uchunguzi wao umebaini
kuwa,eneo la kuoshea chupa ni chafu na kwamba chupa hizo zimekuwa zikioshwa
katika mazingira yasiyoridhisha.
Alisema wamiliki wa kiwanda hicho
wamepewa muda wa kurekebisha kasoro hizo na baada ya kufanya hivyo TFDA
itafanya ukaguzi tena kujiridhisha kama kasoro hizo zimefanyiwa kazi,
Katika hatua nyingine,jeshi la
polisi kwa kushirkiana na maofisa wa mamlaka ya mapato
Tanzania(TRA),wamefanikiwa kukamata shehena ya vifungashio vinavyotumiwa
na kampuni moja mkoani Shinyanga ya Canon General Supply inayojihusisha na utengenezaji wa pombe kali
aina ya Shujaa.
Vifungashio hivyo vilikamatwa ndani
ya kiwanda hicho kilichopo eneo la Kwa Alphone kata ya Kiborironi huku baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho
wakishikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.
Akizungumzia tukio hilo,ofisa huyo
kutoka TFDA alisema hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria inayosimamia usajili wa
bidhaa na kuongeza kuwa,vifungashio vilivyokamatwa ndani ya kiwanda hicho
havimo kwenye orodha ya usajili wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Moja ya vifungashio vilivyokamatwa na polisi katika kiwanda cha D.G.T cha mjini Moshi,vifungahio hivyo ni mali ya Kampuni ya Canon General Supply ya mjini Shinyanga.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa
Kilimanjaro,Hamisi Issah alisema jeshi hilo linamshikilia meneja wa Kiwanda
hicho aliyemtaja kwa jina la Boniface Damas(56) pamoja na wafanyakazi watatu wa
kiwanda hicho.
Kamanda Issah aliwataja wafanyakazi
hao kuwani Severine Pantaleo(37),Riziki Fabian (28) na Daniel Japhet(18) ambao
wanadaiwa kukutwa na pombve kali iliyofungashwa kwenye viroba iana ya Zed
inayodaiwa kutengenezwa kienyeji.
“Viroba hivyo vina alama zake,lakini
watuhumiwa hawa walikuwa wakitengeneza katika mfumo wanaoujua
wenyewe,utengenezaji wa pombe usiozingatia taratibu ni hatari na unaweza kuleta
madhara makubwa kwa wanywaji”,alisema kama Issah.
Kuhusu
vifungashio vilivyokamatwa ndani ya kiwanda cha D.G.T,kamanda Issah alisema
kuwa,wamiliki wa kiwanda hicho hawakuwa na haki stahiki ya kutengeneza pombe
hizo kutokana na kutengeneza pombe hizo pasipo kuzungitia tararibu za kisheria.
Kamanda
Issah amesema polisi kwa kushirikiana na TFDA wanafanya uchunguzi juu ya tuhuma
hizo ikiwamo matumizi ya malighafi isiyo ya kiwanda hicho na uchunguzi
ukimalika shweria itachukua mkondo wake kwa watakaobainika kutenda makosa.
Meneja wa Kiwanda cha Derrick Global Trading(D.G.T) cha mjini Moshi,Boniface Damas(kulia)akiwa ndani ya gari la polisi na watuhumiwa wenzake baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kutengeza pombe kali kwa kutumia vifungashio vya kampuni ya Canon General Supply ya mjini Shinyanga kinyume cha sheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni