NA CHARLES NDAGULLA,HAI
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani
Kilimanjaro(TAKUKURU) imetoa onyo kwa watumishi wa umma kuacha kuchezea fedha
za serikali na atakayejaribu ataishia pabaya ikiwamo kufikishwa makahamani.
Onyo hili la Takukuru linakuja siku
chache baada ya kuwafikisha makahamani watumishi saba wa Halmashauri ya wilaya
ya Hai kwa tuhuma za kujihusisha na ufujaji wa fedha za umma.
“Takukuru tunasisitiza kuwa hakuna
mbadhilifu wa fedha za umma mkoani Kilimanjaro atakayeabaki salama,ni suala la
muda tu,hivyo ni rai yetu kuwa wenye fikra za kufanya ubadhilifu ni bora
wakaacha mara moja na kujifunza kiridhika na vipato vyao halali au wakaacha
kazi za umma wakatafute kazi zenye maslahi wanayodhani yatakidhi matamanio yao “,ni
onyo la Mkuu wa takukuru,Holle Makungu
Watumishi hao wameshitakiwa kwa
makosa ambayo yanafanana ya wizi na ubadhilifu na baadhi yao wamejikuta
wakiburuzwa mahamani mara tatu kwa makosa hayo hayo ya ufujaji wa fedha za
umma.
Aliyeanza kuonja joto ya jiwe ni
Thadeus Theobald Meela ambaye alikuwa mweka hazi wa halmashauri hiyo wakati wa
ufujaji wa fedha hizo kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Ruangwa na baadaye Pangani
mkoa wa Tanga.
Meela alijikuta akiunganishwa tena
katika mashitaka ya wizi na ubadhilifu wa fedha hizo za umma na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bariadi
mkoani Simiyu ,Melkizedeck Oscar Humbe pamoja
na karani wa fedha,Valentina Elisha Mollel .
Watatu hawa wameshitakiwa kwa kosa
la wizi na ubadhilifu wa zaidi ya shilingi Milioni 27wanaodaiwa kuufanya mwaka
2014 wakati huo Humbe akiwa Mkuregenzi wa halmashauri hiyo.
Takukuru katika kuonyesha
haitanii,safari hii imemfikisha mahakamani Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa
Kigoma(RMO) Dkt. Paul Christopher Chaote akishitakiwa na wenzake watano kwa
makosa 109 ya ubadhilifu wa fedha wa zaidi ya shilingi Milioni 38 na kusaidia kutendeka kwa kosa pamoja na
kuandaa nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya mwajiri.
Wengine ni Philipo Alexander
Masasi,Thadeus Theobald Meela,Christopher Nyamagera Manzi,Edwid Mtalemwa
Kalokola na Valentina Elisha Mollel ambao wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya
oktoba 2014 na januari 2015.
Walifikishwa mbele ya hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Hai,Arnold Kirekiano na kusomewa mashitka na
waendesha mashitaka wa Takukuru,Rehema Mteta akisaidiana na Suzan Kimaro.
Wanadaiwa kwa matumizi mabaya ya nyaraka
ikiwamo kuandaa nyaraka za uongozi kwa lengo la kumdanganya
mwajiri,ubadhilifu na kusaidia kutenda
makosa ambako wanadaiwa kutumbua kiasi hicho cha fedha zilizokuwa kwa ajili ya
posho ya kuitwa kazini kwa madaktari(on Call allowance) katika hospital ya
Machame .
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka,washitakiwa hao wenaidaiwa kuwa,mnamo Oktoba mwaka 2014 kwa pamoja wakiwa watumishi wa halmashauri ya wilaya ya hai, kwa njia za udanganyifu walijimilikisha kiasi cha sh,Milioni 19.200,000 zilizokuwa kwa ajili ya posho ya kuitwa kazini kwa madaktari na wauguzi katika Hospital ya Machame.
Baada ya washitakiwa hao kuzitafuna
fedha hizo ndipo walipoandaa nyaraka mbali mbali kuonyesha kuwa fedha hizo
zililipwa kwa madaktari na wauguzi wa Hospital hiyo ya Machame kama posho ya
kuitwa kazini kwa madaktari hao na wauguzi jambo ambalo halikuwa kweli .
Baada ya kusomewa mashitaka
hayo,washitakiwa Paul Chaote, Thadeus Meela, Valentina Molle na Christopher Manzi walikana mashitaka yao huku washitakiwa wengine wawili,Phillipo Alexander
Masasi na Edwin Mtalemwa Kalokola wakiingia mitini .
Washitakiwa hao wapo nje kwa dhamana
hadi Februari 15 mwaka 2018 kesi yoa itakapokuja kwa ajili ya kutajwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana
yaliyowataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosai bondi
ya milioni 5, kila mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni