Ijumaa, 12 Desemba 2014

UVUNAJI WA MBAO, WATEKETEZA MISITU LUSHOTO



Z
aidi   ya wananchi 1000 wanaoishi kuzunguka msitu wa asili wa Bombo makole uliopo wilayani hapa wapo hatarini kukosa maji  kutokana na tishio la kukauka kwa vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji kwa wananchi hao kutoka katika msitu huo.

Tishio hilo la kukauka kwa vyanzo vya maji linatokana na kasi ya uvunaji  haramu wa mbao kutoka katika msitu huo unaofanywa na wafanyabiashara kwa kushirikiana na maofisa misitu wasio waaminifu wanaodaiwa kutoa vibali vya kuvuna magogo katika msitu huo kwa kisingizio cha shughuli za maendeleoe.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi  kwa zaidi ya wiki mbili wilayani hapa,umebaini kuwa,halmashauri ya wilaya ya Lushoto kupitia amati ya uvunaji imekuwa ikitumia mwanya huo kushirikiana na wafanyabiashara uhumu msitu huo.

Msitu huo ambao upo chini ya Halmashauri ya wilaya ya Lushoto umekuwa kichocheo kikubwa cha upatikanaji wa maji kutokana na kusheheni miti ya asili inayowezesha upatikanaji wa maji kwa mwaka mzima .

Akizungumza, mwenyekiti wa kijiji cha makole kilichopo kata ya Kilole,Athuman Tupa,alisema kuwa kama hatua madhubuti hazitachukuliwa uuokoa msitu huo,wananchi wa vijiji hivyo wataathirika kwa kiwango kikubwa na ukosefu wa maji.

Alisema kuwa,licha ya halmashauri ya wilaya ya Lushoto kuwachagisha fedha wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule,wananchi wa maeneo hayo hawanufaiki na raslimali za msitu huo kutokana na kuwanufaisha watu waliopo nje ya eneo lao.

Naye diwani wa kata ya Kilole,Salehe Manyenya,alisema kuwa pamoja na uvunaji huo wa magogo kuendelea,shule nane za msingi zilizopo kuzunguka msitu huo,zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati licha ya halmashauri ya wilaya kudai kuwa magog hayo yanavunwa kwa ajili ya matengenezo ya madawati.

Alizitaja shule hizo kuwa ni MziMkuu, Kwekanga, Makole, Ngwelo, Kwemanoo, Hemtoye, Chaumba ba Kwedeghe ambazo baadhi ya wanafunzi wamekauwa wakisoma huku wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba huo wa madawati.

Hata hivyo ofisa msitu wilaya ya Lushoto,Rashirid Hassan alikataa kuzugumzia shutuma hizo kwak ile alichodai yeye si msemaji wa halmashauri licha ya nyaraka kuonyeshe kuwa yeye ndiye mmoja wa maofisa wa idara ya misitu ambao wamekuwa wakitoa vibali vya ununaji wa magogo.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo mwandishi anazo,desemba 2 mwaka jana ofisa misiti huyo alitoa vibali  viwili kwa watu waliotajwa kwa majina ya  Kumbula Mbangula na Bebwa G.Ludovick kwa ajili ya uvunaji wa aina ya mikaratusi vibali ambavyo wananchi hao wanadai kuwa vinatumika kwa ajili ya kukata miti ya asili na si mikaratusi.

Hata hivyo vibali hivyo vinaonyesha waliopewa wanaruhusiwa kukata miti kwa ajili ya shughuli za maenndeleo na shughuli binafsi vibali ambavyo havifafanui shughuli binafsi ni zipi  na shughuli za maendeleo ni zipi.

NORTHERN HIGHLANDS TEACHERS COLLEGE, HAPAFAI!!!!



U
salama wa wanafunzi wanaosoma katika chuo cha ualimu cha Northern Highlands Teachers College mjini Moshi upo mashakani kutokana na hofu ya kuangukiwa na miti iliyoshikizwa katika jengo hilo .
 Muonekano wa jengo la chuo cha ualimu cha Northern Highlands mjini Moshi, upande wa mbele


Wakizungumza, wanafunzi hao bila kutaja majina yao, wamedai kuwa, hofu ya usalama wao inatokana na ukweli kwamba,licha ya jengo hilo kutokamilika kwa aslimia 100, hadi sasa ndilo linalotumika kama madarasa na hapo hapo linatumika kwa ajili ya makazi yao.

Wamedai kuwa, Novemba 22 mwaka huu wanafunzi sita walilazwa katika Hospital binafsi ya Kilimanjaro iliyopo mjini hapa baada ya kupata mshituko uliotokana na kuanguka kwa moja ya tofari lililokuwa juu  ya jengo hilo na hivyo kuibua taharuki iliyosababisha wenzao kulazwa kwa siku mbili kwa matibabu.
Hata hivyo,katika kuficha ukweli,mmoja wa wakurugenzi wa Bodi ya chuo hicho, Henry Mallya, alikana kata kata kuwepo kwa tukio hilo ikiwamo wanafunzi hao kulazwa hospitalini lakini baada ya waandishi kuanza kupiga picha za jengo la chuo hicho,alianza kuwapigia simu na kuwasihi wasitoe habari za tukio hilo.

Mallya alikutana na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki ofisini kwake iliyopo shule ya sekondari ya Norther Highlands ambako alikana kuwapo kwa tukio hilo, lakini baada ya nusu saa Mallya huyo huyo aliwapigia simu tena waandishi wa habari akiwasihi wasichapishe picha za jengo la chuo hicho baada yak upewa taarifa za wasaidizi wake juu ya picha hizo kupigwa.
Kwa mara ya pili Mkurugenzi  huyo ambaye pia anamiliki shule ya msingi ya The Moshi Academy, aliwaita waandishi wa habari kwenye ofisi yake iliyopo kwenye majengo ya shule hiyo ya msingi na kuwasihi wasichapishe habari au picha za chuo hicho akihofia ushindani wa kibiashara na licha ya kuelezwa kuwa waandishi wa habari hawafanyi biashara, alisisitiza kutochapishwa kwa habari hizi.

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA MAJENGO SECONDARY ATOWEKA KUSIKOJULIKANA



M
wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari majengo,Said Seleman (14) mkazi wa mtaa wa Arabika kata ya Majengo Manispaa ya Moshi, ametoweka nyumbani kwao kwa zaidi ya miezi miwili sasa huku familia yake ikipoteza matumaini ya kumpata kutokana na kutoonekana kila kona wanayomsaka.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa mwanafunzi huyo,salama saidi,kijana huyo alitoroka nyumbani kwao Oktoba nane mwaka huu wakati mama yake akijiandaa kwenda na mwanafunzi huyo shuleni kwao kutokana na kutuhumiwa kutenda utovu wa nidhamu.

Akizungumza na blog hii, mama huyo alisema tangu siku hiyo wamekuwa katika harakati za kumtafuta mwanaye bila kafanikio na kuomba watu wenye mapenzi mema ambao watafanikiwa kumuona mwanaye watoe taarifa kituo chochote cha polisi au wampige simu yake ya kiganjani namba 0754 03 63 12.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa mwanafunzi huyo, mwanaye alikuwa akituhumiwa kujihusisha na wizi wa mabegi ya wanafunzi wenzake na kwenda kuyauza na kisha kugawana fedha na wanafunzi wenzake na baada ya arobaini yake kufika siri ikafichuka na kubanwa ili ataje washirika wake.

Pia alisema, sakata hili lilifikishwa nyumbani kwao na mama huyo akashauri likazungumzwe kwa uwazi shuleni na ndipo kijana huyo alioingiwa na hofu na kisha kutimka kutokana na kuonywa na wenzake kuwa akikamatwa ni marufuku kuwataja washirika wake.

Tayari mama huyo ametoa taarifa za kupotelewa na mwanaye katika kituo cha polisi majengo ambako jarada limefunguliwa na kupewa namba MAJ/RB/3513/2014.

Hima hima wananchi kwa atakayemuona mwanafunzi huyo atoe taarifa zitakazosaidi kupatikana kwake kwani kwa kitendo chake cha kutoroka nyumbani amekosa fursa ya kufanya mtihani wa kidato cha kwanza na hivyo kuwa katika hatari ya kukosa nafasi ya kusonga mbele  kwa kidato cha pili

KUBADILISHA VIWANGO VYA UFAULU MARA KWA MARA, CHANZO CHA KUDIDIMIZA ELIMU



W
adau wa elimu nchini   wameishutumu serikali  kwa kubadilisha mara kwa mara viwango vya ufaulu bila kufanya tathmini ya kutosha mpango uliofananishwa na upanuzi wa magoli ili kumwezesha kila mchezaji kufunga kirahisi.

Shutuma hizo zilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa shule ya sekondari Majengo iliyopo chini ya kanisa Katoliki Jimbo la Moshi,Peter Lyimo katika hotuba yake kwenye mahafali ya 28 ya wahitimu 568 wa kidato cha nne .

Br.Peter Lyimo
Mwalimu mkuu  wa shule ya sekondari Majengo
Alisema kuwa hali hiyo ni ya hatari na kmwaba inaua elimu na taifa haliwezi kuendelea kwas mfumo huo na kushauri serikali kuiboresha elimu ili iweze kuandaa wanafunzi kuweza kujitegemea .

Aliitaka serikali kuziboresha shule za ufundi na kuzipa msukumo wa pekee akiamini kuwa ni mhimu sana kwani zinawezesha kuzalisha kazi badala ya kufatufa kazi.

Mkuu huyo wa sekondari majengo alisema kuwa,elimu ya tanzania  haiwezi kuwa bora kama wananchi hawataimiliki  kwa mchango na uwajibikaji na kuongezak uwa kama taifa na jamii yanahitajika mabadiliko ya kifikra  na kimtazamo kuhusu elimu .

“Ndugu zangu,tunatakiwa kuchangia elimu yetu ili iwe bora ,kuna wanafanzi wengi ambao wanashindwa kusoma kutokana na kukosa msaada tunakumbuka kwamba kila mmoja wetu hapa amefika alipo kwa kutembea mgongoni mwa mtu mwingine,baba,mama,mjomba,shangazi,ndugu n.k”alisema.

Alisema pamoja na  kubadili viwango vya ufaulu na kuwa na daraja la tano, bado tatizo la ajira lipo palepale na zaidi ya yote linazidi kuwa kubwa zaidi kutokana na wengi wa wanaohitimu vyuo vikuu kutokuwa na ujuzi na kuongeza kuwa endapo shule za ufundi zingepewa kipaumbele tatizo hilo lingepungua .

Alionya kuwa kwa kutopewa kipaumbele elimu ya ufundi  ni mzigo ambao serikali inajitakia kwani endapo ingetilia mkazo  elimu hiyo ,kila mhitimu anayehitimu chuo kikuu angeweza kuwa na ujuzi na kujiajiri wenyewe  badala ya kusubiri kuajiriwa.

Aidha Lyimo aliiasa jamii kubadilika  kifikra kwa kuwekeza katika elimu badala ya kuwekeza kwenye harusi jambo ambalo haliisaidii jamii na badala yake elimu inazidi kushuka siku hadi siku na kupelekea tatizo la ajira kuzidi kuwa kubwa.