Jumatatu, 3 Novemba 2014

MTANZANIA ATESWA DUBAI


 MWANAISHA ATHUMANI PINDE

Usalama  wa watanzania wanaopelekwa nchini Dubai  na Falme za Kiarabu kujaribu fursa za ajira upo shakani kutokana na baadhi ya waajiri nchini humo kuwafanyia vitendo visivyokuwa vya kibinadamu ikiwamo kupokwa pasi zao za kusafria na wengine kujikuta wakiswekwa jela bila hatia.

Uchunguzi uliofanywana mtandao huu kwa zadi ya mwezi mmoja sasa umebaini kuwa mbali na hilo,watanzania hao wamejikuta wakifanya kazi kwa mali kauli pasipo kulipwa mishahara yao kama ambavyo mikataba ya ajira inavyoosha.


Mmoja wa wahanga hao ni binti mwenye umri wa miaka 36 ,Mwanaisha Athuman Pinde aliyezaliwa mkoani  Morogoro Novemba 25 mwaka 1978 kama pasi yake ya kusafiria inavyoonyesha.

Kwa mujibu wa nyaraka tulizonazo,Mwanaisha aliondoka Jijini Dar e s salaam kwenda Dubai  Februari 17 mwaka huu na ndege ya shirika la ndege la Qatar yenye namba QR1350.

Uchunguzi umebaini kwamba alisafiri kwa msaada wa kampuni ya Bravo Job Centre Agency Ltd ya Jijijini Dar es salaam inayojihusisha na kuwatafutia fursa za ajira watanzania katika nchi mbalimbali na kupokelewa na wakala aitwaye Oriental Int,Labour Supply aliye na mkataba na Bravo.

Habari zinadai kuwa,baada ya binti huyo kupokelewa na kupelekwa kwa mwajili wake,alijikuta akiingia kwenye mgongano na mama mwenye nyumba na kulazimika kusitisha mkataba na kupelekwa kwa mwajili mwingine.

Kwa mujibu wa dada wa binti huyo,Zena Athuman Pinde,mdogo wake huyo baada ya kupelekwa kwa mwajili mwingine aliipokwa pasi yake ya kusafiria,simu pamoja na nyaraka nyingine huku akinyimwa kufanya mawasiliano na ndugu zake.

Zena alisema kuwa,mbali na hilo mdogo wake alikuwa akiishi bila kulipwa mshahara na pale alipodai mshahara wake alijikuta akiambulia lugha chafu kutoka kwa mwajili wake.

Kwa upande wake Mwanaisha akiongea na mwandishi wa habari hizi  kwa njia ya simu kutoka Abu Dhabi hivi karibuni,alisema alijikuta akiswekwa jela na maofisa wa polisi wa huku baada ya mwajili wake kumtelekeza na kushidwa kumrejesha nyumbani huku pasi pake akiwa ameishilikia pamoja na simu yake ya kiganjani.

Akizungumza kwa msaada wa ofisa wa polisi mwenye asili ya Tanzania,mwanaisha amedai kuwa,chanzo cha kutofautiana na mwajili wake ni hatua ya bosi huyo kutaka kumgeuza kitega uchumi kwa kumbadilisha kazi za ndani na kutaka kumtumia katika biashara haramu.

Amedai baada ya kugoma,alijikuta katika mgogoro na bosi wake na hapo upepo ukawa mbaya kwake kwani alijikuta akipokwa kila kitu huku akiwa hajalipwa mshahara wake kwa muda wa miezi sita sasa.

kwa mujibu wa mwanaisha,tangu awasili Abu Dhabi,amekuwa hana mawasiliano na ndugu zake kutokana na simu yake kuwa mikononi mwa bosi wake japo amefanikiwa kurejea nyumbani kwa msaada wa ubalozi mdogo wa tanzania huko Abu Dhabi baada ya kupatiwa hati ya muda ya kusafiria.

Akizungumza muda mfupi baada ya kurejea nchini hivi karibuni na ndege ya shirika la ndege la kenya na kupokelewa na ndugu zake,mwanaisha anadai kwa sasa anakamilisha tararibu za kisheria kuifikisha mahakamani kampuni ya Bravo kwa kile alichodai kushindwa kumsadia kupata haki zake.

Hata hivyo,msemaji wa kampuni hiyo ya Bravo,Heri Mtemvu akizungumza na mtandao huu hivi karibini ofisini kwake Keko Bora jijini Dar es salaam,alitetea hatua ya waajili huko Dubai ya kuwapoka simu na pasi za kusafiiria watanzania wanaokwenda kufanya kazi huko.

Kwa mujibu wa Mtemvu,hatua ya kupokonywa pasi na simu ni katika juhudi za kuzima majaribio ya watumishi hao kutoroka pindi wanapopata vibali vya kuwawezesha kufanyakazi nchini humo.

Mtemvu hata hivyo alisema,kampuni yake ipo katika hatua za mwisho kwenda nchini Dubia kufuatilia haki za mtanzania huyo ikiwamo mishahara yake pamoja na pasipoti yake ya kusafiria ambayo ingali mikononi mwa tajili yake.

Kwa mujibu wa nyaraka tuliozonazo,safari za watanzania kwenda katika nchi za falme za kiarabu zimekuwa zikipata baraka kutokana wakala wa Huduma za ajira Tanzania(TaESA) ambako mhusika hulipia ada ya sh,100,000 .

Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa,mwanaisha alikuwa na mkataba  wa kufanyakazi za ndani kwa  mfanyabiashara Mohamed Saleh Yeslam Alameri ulioidhinishwa februari 5 mwaka huu na kutiwa saini na Omary Mjenga kutoka TaESA.

"mtajwa hapo juu mwenye pasipoti namba AB474488 amethibitishwa na ubalozi wa tanzania ulioko Dubia,UAE kwmaba amepata kazi nchini humo,wakala wa huduma za ajira tanzania umeridhia utaratibu uliotumika kwa kumuunganisha  mtajwa hapo juu na fursa ya ajira",inasema barua ya TaESA.

Barua hiyo iliyotumwa uhamiaji kwa taratibu zadi ya kiuhamiaji,ilisainiwa na K.V.Kilindu  februari 12 mwaka huu kwa niaba ya mtendaji mkuu wa TaESA huku ikiwa imebandikwa picha ya mwanaisha.

kwa mujibu wa mkataba ambao nakala yake tunayo,mwanaisha alikuwa alipwe mshahara wa AED 1100  sawa na sh,460,000 za tanzania lakini kwa mujibu wa maelezo yake,alielezwa kuwa atalipwa AED 800 sawa na sh,360,000 ambazo hata hivyo alidai hajawahi kulipwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni