Jumatano, 26 Novemba 2014

UVAMIZI VYANZO VYA MAJI UNACHANGIWA NA WATENDAJI WABOVU



Uvamizi  yanaofanywa na watu  kwenye vyanzo vya maji katika naeneo mbalimbali ya mji wa moshi yanatokana na matunda ya uongozi mbovu wa watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia sheria za mazingira katika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya moshi.
MEYA WA MANISPAA YA MOSHI, JAPHARY MICHAEL
Tuhuma hizo zilitolewa  na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Japhary Michael katika mkutano wake na waandishi wa habari uliolenga kuelezea hali halisi ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa manispaa hiyo na changamoto zinazoikabili mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira moshi mjini(MUSWA).

Meya huyo alisema kuwa upo ulegevu katika suala zima la utekelezaji wa sheria ambao umesababisha watu kujenga karibu na vyanzo vya maji kikiwamo chanzo cha maji cha Njoro ya |Dobi ambacho katika miaka 15 iliyopita,chanzo hicho kilikuwa moja ya vyanzo mhimu vya maji katika mji wa Moshi.

Alisema kuwa chanzo hicho kimevamiwa na watu  na kuweka makazi ya kudumu licha ya kelele za watetezi wa mazingira na kuongeza kuwa uvamizi huo umechangiwa na wenye mamlaka ya kusimamia sheria kutokuchukua hatua stahiki.

Kwa sasa chanzo hicho cha maji hakitumiki kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuvamiwa na wananchi waliojenga nyumba za makazi ambako wamekuwa wakitiririsha maji machafu yanayotokana na kinyesi cha binadamu hali ambayo imekiweka chanzo hicho katika mazingira hatarishi.

Kuhusu ujenzi holela unaoendela katika baadhi a maeneo ya mji wa moshi,mtahiki meya huyo alisema kuwa,ujenzi huo holela unashika kasi kutokana na usimamizi mbovu wa watendaji wa manispaa ya moshi ambapo shutuma hizo alizielekezam oja kwa moja kwa idara ya mipango miji ambayo ndiyo yenye wajibu wa kuhakikisha ujenzi holela unadhibitiwa.

Kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika mji wa moshi,meya huyo alisema kuwa,kwa sasa kuna jitihada kubwa zinazofanywa na MUWSA katika kutatua tatizo la maji kwa wakazi wam ji wa moshi huku maoneo yaliyokuwa yakikabiliwa namgao mkubwa wa maji kama vile Kiboriloni,Msaranga,pasua na Bomambuzi,maeneo hayo kwa sasa yanapata maji ya kutosha.

Hata hivyo, Meya huyo alisema kuwa,yapo baadhi ya maeneo ambayo bado hayapati maji ya uhakika na kwamba hiyo ni changamoto kwa MUWSA kuhakikisha maeneo hayo yanapata maji ya kutosha huku akielezea matumaini kwa wakazi wa kata za pasua na Bomambuzi ambao kwa sasa wananufaika na mradi wa maji kutoka chanzo cha maji cha mto karanga.

Alitoa wito kwa wakazi wa manispaa ya moshi kuwa mabalozi wazuri katika kusimamia ulinzi wa miundombinu ya maji ikiwamo pia kuwa na matumizi mazuri ya maji safi na salama na kuzuia upotevu huo wa maji.

Akizungumzia mfumo wa maji taka,meya huyo alisema kuwa bado jamii ya wananchi wa mji wa moshi hawajapata elimu ya kutosha juu ya kuunganishwa kwenye huduma hiyo na kuongeza kuwa hiyo ni changamoto kwa MUWSA na manispaa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuunganishwa katika huduma hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya MUWSA, mji wa moshi umegaswanywa katika kanda kuu tisa ambako kila kanda inapata maji kwa wastani wa saa 18 hadi 24 kutegemea na eneo lilivyo ambako katika kipindi cha julai 2013 hadi sasa,wastani wa kutoa huduma ya maji kwa wateja umeimarika kutoka saa 17.3 hadi saa 21.5.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni