Alhamisi, 1 Machi 2018

MAJANGILI WALIOUA FARU SERENGETI WANASWA


ASKARI  wa shirika la Hifadhi za taifa nchini(Tanapa)wakishirikiana na askari wa jeshi la polisi nchini,wamefanikiwa kuwanasa watu wanne  wanaotuhumiwa kuwa ni majangili wanaodaiwa kujihusisha na mauaji ya wanyama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti(SENAPA).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kupitia Meneja mawasiliano,Tanapa Pascal Shelutete leo machi mosi,imeeleza kuwa,miongoni mwa majangili walionaswa ni wale wanaodaiwa kuua faru katika hifadhi hiyo mwezi Desemba mwaka jana.

Mbali na kukamatwa kwa majangili hao,pia katika kamata kamata hiyo ilifanikisha kukamatwa bunduki aina ya Lifle 458 inayodaiwa kutumika katika tukio hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni